TAFIRI NA FETA ZAAGIZWA KUZALISHA VIFARANGA MILIONI 10 VYA SAMAKI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA) kufanya utafiti na kuongeza uzalishaji wa vifaranga vya samaki milioni 5 kila mmoja kwa mwezi ili kupunguza changamoto ya gharama kubwa ya upatikanaji wa vifaranga kwa wafugaji wa samaki.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ametoa agizo hilo Agosti 15, 2026 wakati wa ziara yake mkoani Mwanza ambapo pia amewataka wawekezaji wakubwa katika sekta ya ufugaji samaki kuongeza uzalishaji wao ili kuwa na mchango mkubwa na kuleta ushindaji katika sekta hiyo
" Wawekezaji wakubwa katika ufugaji wa samaki lazima ukubwa wao katika uzalishaji watofautiane na wale wadogo. sitatoa kibali kwa wawekezaji wakubwa wanaofuga samaki wa mboga kama wafugaji wadogo wa samaki" alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.
Katika hatua nyingine Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameiagiza TAFIRI kufanya utafiti utakaosaidia kidhibiti na kulinda mazingira na fukwe za Ziwa Victoria ambapo ameitaka taasisi hiyo kishirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza ili kutathmini na kuja na suluhisho la kulilinda ziwa hilo ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa sheria.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amesema kupitia programu ya utoaji wa mikopo halmashauri, Wilaya hiyo imetoa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana kufuga samaki kwa njia ya vizimba hatua ambayo imeongeza hamasa na mwamko wa ufugaji wa samaki katika wilaya hiyo.