SERIKALI KUTUMIA BILIONI 1.6 KUKARABATI KITUO CHA VIUMBE MAJI RUHILA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema wizara yake ipo katika taratibu za kupata mkandarasi wa kukarabati kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji Ruhila kilichopo mkoani Ruvuma kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 ili kituo hicho kitumike kutoa huduma za ufugaji wa samaki katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe na Mbeya.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, mkoani Ruvuma, ziara inayolenga kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo iliyofanyika leo Novemba 11, 2026.
Katika hatua nyingine, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema Wizara hiyo, imeendelea kutekeleza maagizo na maelekezo ya Makamu wa Rais kuhusu changamoto katika sekta za mifugo, ambapo amesema Mawaziri wa Sekta Nane wameendelea kufanya vikao vinavyolenga kutatua changamoto za sekta hiyo ili kuhakikisha shughuli za uzalishaji ikiwemo ufugaji zinaendelea kufanyika kwa amani na usalama kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Ziara hiyo, itaendelea kesho Novemba 11, 2026 katika Wilaya ya Namtumbo na Tunduru mkoani Ruvuma na Baadae Masasi Mkoa wa Mtwara.