Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MIFUGO NA UVUVI KINARA WIZARA ZA KISEKTA NANENANE 2026

Imewekwa: 11 August, 2026
MIFUGO NA UVUVI KINARA WIZARA ZA KISEKTA NANENANE 2026

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa pili mfululizo imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa upande wa Wizara za kisekta kwenye Maonesho ya kitaifa na kimataifa ya NaneNane kwa mwaka 2026.

Wizara imepata ushindi huo kutokana na kuongoza kwenye vipengele mbalimbali ikiwemo ubunifu wa teknolojia rafiki kwa matumizi ya wadau wote wa sekta za Mifugo na Uvuvi.

Aidha miongoni mwa matukio bunifu yaliyoipa Wizara hiyo ushindi huo ni teknolojia ya malisho ya Mifugo aina ya Juncao, kilimo mseto cha Mpunga na samaki, Paredi ya Mifugo iliyokuwa na rekodi ya Ng’ombe mwenye uzito wa kilo 922, Mnada wa Mifugo ambao kwa mwaka huu ulishuhudia ng’ombe wawili wakiuzwa kwa shilingi Mil.22 na Kijiji cha Protini ambacho kilikuwa kivutio cha wengi kutokana na upatikanaji wa mazao yote ya protini itokanayo na samaki na wanyama.

Mbali na Ushindi huo wa Wizara, Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo zimefanikiwa kufanya vizuri kwenye Maonesho hayo ambapo Wakala ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA) ilishika nafasi ya pili huku Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) zikishika nafasi ya 3 kila moja kwenye kundi lake.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo