Mhe. Luhaga Mpina ampongeza Bw. Paul Kimiti Mwenyekiti wa Bodi ya (NARCO) baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais.

Imewekwa: Monday 29, October 2018

YALIYOJIRI LEO OKTOBA 27, 2018 WAKATI WA UZINDUZI WA BODI YA KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO)*

#Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imezinduliwa rasmi leo tarehe 27/10/2018 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina.

#Ninawashukuru wote kwa kukubali uteuzi huu kwa sababu natambua hakuna kazi iliyo nyepesi - Waziri Mpina

#Namshkuru Mhe. Rais Magufuli kwa uteuzi huu kwani ametambua uwezo na uzalendo wenu, Nchi hii inapaswa kuendelezwa na wananchi wazalendo watakaowezesha Nchi kusonga mbele - Mhe. Mpina

#Ni matarajio yangu kuwa;

Bodi hii itaweza kufikia Mikakati tuliojiwekea na ndani ya Wiki mbili zijazo lazima kikao cha Bodi kiitishwe ili kuanza utekelezaji wa mikakati tutakayojiwekea - Waziri Mpina

#Sekta ya Mifugo ina mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa letu ambapo mpaka sasa jumla ya Mifugo tuliyonayo ni mil 57 na tunazalisha Lita Bil 2.4 za Maziwa - Waziri Mpina.

#Tunahitaji mpaka mwakani tuongeze idadi kubwa ya Mifugo kwa sasa, tuna Ng'ombe milioni 30.5, mbuzi 18.8 mil, kondoo Mil. 5.3, nguruwe Mil. 1.9, Kuku wa kienyeji Mil. 38.2, na wa kisasa ni Mil. 36.6.

#Mpaka sasa mifugo inayouzwa Nje ya Nchi kwa njia haramu na halali ni asilimia 70 na mifugo michache tuliobaki nayo ni asilimia 30 - Waziri Mpina.

# Mazao mengi yanaingia Nchini bila kufuata taratibu na Mifugo inatoroshwa kwakuwa hatuna Viwanda vya uhakika hapa Nchini, tuna viwanda 32 lakini ni machinjio- waziri Mpina.

#Ifike mahali kwenye Taasisi za Serikali ikiwemo na NARCO Kuwe na viwanda vya uhakika Itakuwa ni mfano na kielelezo kwa Sekta binafsi - Waziri Mpina.

# Tumepandisha tozo kuanzia 1000 hadi 10,000 ili kila mmoja aweze kumiliki eneo ambalo anauwezo nalo - Mpina.

#Shirika lifike mahali linatoa nyama ya ng’ombe ndani na Nje ya Nchi na kutengenza bidhaa zitokananzo na ngozi - Mpina

#Naitaka Bodi na timu nzima ya kuhakikisha mnaandaa mpango kazi na wa biashara kwa kushirikiana na Dawati la Sekta Binafsi - Waziri Mpina

# kwa mashirika yangu yote kabla ya tarehe 30/11/2018 lazima tuandae gawio letu kwa Serikali - Mpina

#Ni lazima kila mmoja afahamu wajibu wake ili tuweze kufikia mafanikio tuliyojipangia - Waziri Mpina

#Watendaji wa Wizara yangu mtakuwa na kazi ya kusimamia mikakati tuliojiwekea inatekelezaa hadi kufikia tarehe 30/11/2018 nipatiwe mikakati hiyo - Mpina.

#Naimani pamoja na magumu haya mageuzi lazima yafanyike “ penye nia Pana njia” - Mpina.

#Bodi inayozinduliwa leo iko kisheria kwa mujibu wa Mashirika ya Umma na. 2 ya mwaka 1992 kifungu cha 9 (1). Natangaza rasmi uzinduzi wa Bodi hii - Waziri Mpina.

.