​MFUMO WA KIELETRONIKI KUONGEZA TIJA NA UFANISI KATIKA KUSIMAMIA BIASHARA YA MIFUGO

Imewekwa: Saturday 11, June 2022

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA) inaendelea kutoa mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa usimamizi na utoaji vibali mbalimbali wa sekta ya mifugo uitwayo (MIMIS) utaongeza tija na Ufanisi kwenye kusimamia biashara ya mifugo.

Hayo yamesemwa na Afisa Mifugo mfawidhi wa Kituo cha ZVC Tabora, Bi. Adelina Mkumbukwa wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika 07 june 2022, katika ukumbi wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza.

"Niwaombe mfuatilie kwa makini mafunzo haya ili tuwe na uelewa wa pamoja juu ya namna mfumo utakavyokwenda kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara kwa sekta ya mifugo" amesema Mkumbukwa.

Bi Mkumbukwa amesema mfumo utasaidia kuwezesha wadau kufatilia kibali husika namna kinavyofanyiwa kazi na wizara itakapofikia sehemu ya kufanya malipo, ambapo mdau atapata "control number" kwenye dirisha lake au kupitia ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenye simu yake.

Naye Daktari kutoka bodi ya nyama kanda ya Ziwa, Dkt. Anthony Msomi amesema mafunzo haya haya ni swala mtambuka na limekuja kwa wakati muafaka ili kuweza kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa vibali kwa wadau wa sekta ya mifugo, kuwapunguzia gharama za utoaji vibali lakini pia kurahisisha muda wa kuchakata hivyo vibali,

"Huu mfumo ni mzuri sana kwetu sisi wataalamu na watumiaji ambao ni wateja wetu kuhakikisha wote kwa pamoja tunalenga kuiweka wizara yetu ya mifugo na idara zake kuiweka katika hali nzuri" amesema Dkt. Msomi.

Pia Dkt. msomi amesema mfumo huo utawezesha kufanya kazi kwa wakati na kuhakikisha yanafanyika vizuri ili kuwezesha kuongeza tija katika kuwaunganisha na wateja wa mataifa ya nje na masoko ya nje na kwa pamoja kuweza kuongeza pato la Nchi.

.
Tanzania Census 2022 Tanzania Census 2022