Katibu Mkuu Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel atembelea shamba la Mifugo Mkoani Mwanza

Posted On: Monday 13, August 2018

Wafugaji wakumbushwa kufuga kisasa.

Wafugaji Mkoani Mwanza wametakiwa kufuga kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na idadi mdogo ya mifugo ili kuweza kupata tija na kufikia uchumi wa viwanda.

Akiongea na wadau mbalimbali wa mifugo katika mnada wa Nyamatara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza hivi karibuni,Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kujifunza mbinu bora za ufugaji ili sekta ya mifugo iweze kutoa mchango stahiki katika upatikanaji wa Mali ghafi za wiwandani.

Aidha Profesa Elisante amewataka wafugajina wadau wote wa sekta ya mifugo kufata sheria za nchi katika kutekeleza shughuli zao ili kuepusha migongano baina yao na mamlaka mbalimbali za nchi.

Hata hivyo profesaElisante Ole Gabriel amewahakikishia wafugaji kwamba serikali kupitia Wizara ya mifugo itahakikisha matatizo mengi ya wafugaji yanatatuliwa kwa wakati ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Pia amesisitizakuwepo kwa matumizi ya mizani ya kupimia ng'ombe na sio kuuza kwa kuangalia ukubwa wa ng'ombe kwa macho ambapoitasaidia mfugaji na mnunuzi na kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya Wizara, wafugaji na wanunuzi wa mifugo ili kuweza kufanya kazi zao katika utaratibu unaoeleweka.

.