KAMPUNI YA OPENIA YAONYESHA NIA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA UVUVI

Imewekwa: Tuesday 28, September 2021

Serikali inatarajia kutangaza zabuni ya ujenzi wa bandari ya Uvuvi hivi karibu ambapo kampuni ya Openia imeonyesha kuvutiwa na imekaribishwa kuomba pindi itakapotangazwa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah Septemba 09, 2021 baada ya kukamilika kwa kikao cha pamoja kati ya watendaji wa shirika hilo na Serikali ya Tanzania iliyowakilishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dodoma.

Aidha Dkt. Tamatamah ameeleza kuwa maeneo ambayo kampuni hiyo Ina utaalam, uzoefu na wanavutiwa yanashabihiana na maeneo ya kipaumbele ya Serikali kama uvuvi wa bahari kuu ambapo Openia wanauzoefu wa kutoa mafunzo na utengenezaji meli, pamoja na Uendeshaji wa makampuni ya Uvuvi ambapo TAFICO ina hitaji mbia

Meneja wa Openia Bw. Chris Pugh amebainisha kuwa kampuni hiyo ina teknolojia ya kisasa ya kuunda boti za wavuvi wadogo kwa gharama ndogo ambapo wapo tayari kufundisha watanzania hususan vijana jinsi ya kutengeneza meli hizo kwa kuleta wataalam naipo tayari kuanzisha karakana ya ujenzi wa maboti hapa nchini.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo wanafikiria pia kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza maboti ya uvuvi ili kuondoa adha hiyo kwa nchi za afrika mashariki.

Mazungumzo hayo yameenda vizuri na Openia inategemea kumleta rais wa Kampuni hiyo ndani ya wiki 2 kwa Mazungumzo zaidi.

.