DKT. BASHIRU AUNDA TIMU KUCHUNGUZA UINGIZAJI MIFUGO YA MADARAJA YA CHINI MACHINJIO YA VINGUNGUTI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa leo Oktoba 08, 2026, wakati akikagua miundombinu ya Machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam amelazimika kuunda timu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha uingizaji wa mifugo isiyo na sifa na yenye madaraja ya chini katika Machinjio ya Mifugo Vingunguti.
Hatua hiyo inajiri baada ya Waziri Mhe. Balozi Dkt. Bashiru kumshuhudia ng'ombe dhaifu akiwa kwenye machinjio hayo, ambaye alionekana kukosa huduma ya maji na malisho.
Amesema uchinjaji wa mifugo lazima uzingatie ustawi wa wanyama, Afya pamoja na sheria na kanununi zilizowekwa ambapo ametoa muda wa siku saba kwa timu aliyoiunda kuwasilisha ripoti kwake ikibainisha, eneo alipotoka ng'ombe huyo, mnada wa awali alikonunuliwa, vibali vya kusafirishiwa na huku akiagiza ng'ombe huyo kupatiwa huduma za kiafya na lishe .
Timu iliyoundwa inaongozwa na Mkuu wa Kituo cha ZVC Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania, Meneja wa Machinjio ya Vingunguti na Daktari wa Mifugo wa Machinjio ya Vingunguti.