DKT. BASHIRU ATOA TAMKO LA SERIKALI KUUFUFUA MNADA WA MIFUGO MAGENA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema wafugaji, pamoja Wafanyabiashara wa mifugo nchini wanatakiwa kushirikiana na serikali katika kudhibiti utoroshaji wa mifugo ili kuiwezesha minada ya mifugo nchini ukiwemo mnada wa Magena ulipo Tarime Mkoani Mara kufanya kazi na kuchochea uchumi wa wananchi na kuchangia mapato ya serikali.
Kauli hiyo ameitoa Agosti 13, 2026 Mjini Tarime baada kufika na kukagua miundombinu ya mnada huobambao kwa sasa haufanyi kazi kufuatia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la utoroshaji wa mifugo na mazao yake kwenda nchi jirani hatua ambayo imekuwa ikiikosesha serikali mapato.
Aidha, amesema Wizara kwa kushirikiana na halmashauri ya Tarime kuangalia na kupanga upya siku kwa ajili ya mnada wa magena ili kuondoa changamoto ya mwingiliano na minada jiradi hususan ya nchi jiradi ili mnada huo ufanye kazi.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema mnada wa Magena kutokufanya kazi si tu unaikosesha serikali mapato bali pia wananchi wakiwemo wajasiriamali wanakosa kipato .