Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
SILINDE ANENA MAKUBWA YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA KWENYE SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI
SILINDE ANENA MAKUBWA YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA KWENYE SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ameweka wazi kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande wa sekta za Mifugo na Uvuvi ambapo ameeleza kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji wa mazao ya sekta hizo kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na takwimu za miaka 3 iliyopita.
Mhe. Silinde amesema hayo kwenye hotuba yake ya kufunga Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani tukio lililofanyika leo kwenye Viwanja vya CCM mkoani Kagera ambapo amebainisha kuwa uzalishaji wa nyama umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 16 huku nchi ikiingiza mapato ya kutosha kutokana na usafirishwaji wa zao hilo nje ya nchi.
“Hata uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita Bil.3.6 za mwaka wa fedha uliopita hadi lita Bil.3.9 na mayai kutoka Bil.3.2 mwaka uliopita hadi Bil.3.9 mwaka huu hivyo unaweza kuona juhudi za wazi za Mhe. Rais Samia katika kuinua sekta za uzalishaji na kuboresha lishe” Ameongeza Mhe. Silinde.
Aidha Mhe. Silinde ameeleza jitihada zilizofanywa na Mhe. Dkt. Samia kwa upande wa sekta ya Uvuvi ambapo amegusia ongezeko la kiwango cha uzalishaji wa samaki kutoka tani laki 4 za mwaka uliopita hadi tani laki 4.3 mwaka huu huku akipongeza jitihada za Wizara katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu.
“Jambo ambalo Dkt. Samia Suluhu Hassan amelifanya sasa hivi, amewekeza katika vizimba kwa wananchi, amewekeza katika utoaji wa maboti kwa mikopo nafuu kwenye makundi na vyama vya ushirika ambavyo vinajishughulisha na uvuvi na anawekeza katika kwenye mnyororo wa thamani kwa maana ya vifaa baridi ambavyo vitasaidia kuondoa upotevu wa mazao ya Uvuvi katika maji yetu hivyo unaona kabisa kila kinachofanyika kinaleta tija” Amehitimisha Mhe. Silinde.
Maadhimisho hayo ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani ambayo yamefikia kilele chake leo yalianza Oktoba 10 mwaka huu na kubebwa na kauli mbiu isemayo “Haki ya Chakula kwa Wote kwa Maisha ya Sasa na Yajayo”