Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
​SERIKALI KUTAFUTA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI WA MUUNGANO WA UMOJA WA MAZIWA KILIMANJARO

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na uvuvi (Sekta ya Mifugo) Tixon Nzunda, amesema Serikali itafanya mpango wa kutafuta ardhi kwa ajili ya Muungano wa umoja wa maziwa Mkoani Kilimanjaro(JE) ili waweze kuzalisha kwa tija.
Hayo amesema jana tarehe 27 aprili, 2022 Wilaya Hai Mkoani humo, wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha Maziwa cha Nronga Women na kutembelea duka la pembejeo za Mifugo la Muungano wa Umoja wa vyama vya Maziwa Mkoa wa Kilimanjaro (JE).
Amesema ni vema Serikali ya Wilaya na Mkoa zihakikishe zinawapatia eneo la kuwekeza kikundi cha wanawake cha Nronga pamoja na Muungano wa umoja wa maziwa mkoa wa Kilimanjaro (JE) ambao unaongozwa na wanawake kwa ajili ya uwekezaji wa Kiwanda cha kusindika Maziwa .
Nzunda alisema Serikali iko mbioni kuondoa baadhi ya kodi kwenye bidhaa za Maziwa ili wasindikaji, ikiwa ni pamoja na ushirika huo wa Muungano wa Umoja wa vyama vya maziwa mkoa wa Kilimanjaro (JE) waweze kuzalisha na kusindika Maziwa kwa tija bila vikwazo vya mlundikano wa kodi.
Aidha, Katibu Mkuu Nzunda aliwataka Maafisa Mifugo kutembelea vyama vya ushirika vya maziwa na kuvijengea uwezo na misingi ya kisheria ya uzalishaji maziwa ili viweze kuzalisha maziwa hayo kwa tija.
"Takribani Miezi mitatu sasa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) imeandaa Mpango Mkakati wa kuibadilisha (Transform) Sekta ya Mifugo ili iweze kuchangia katika Pato la Taifa, na moja ya eneo lililopewa kipaumbele ni pamoja na tasnia ya maziwa". Alisema Nzunda.
Aidha, aliupongeza Muungano wa Vyama vya Maziwa mkoa wa Kilimanjaro (JE) kwa kuwezesha wanachama kupata huduma za ugani kwa kuanzisha duka lenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni, pamoja na kuanzisha kiwanda cha kuchakata chakula cha Mifugo.
Mwenyekiti wa Muungano wa umoja wa vyama vya maziwa mkoa wa Kilimanjaro (JE) Nancy Mwanasikidi, amesema changamoto wanayokabiliana nayo ni uwepo wa wafanyabiashara wanaouza maziwa bila kuzingatia sheria na taratibu za maziwa hali inayopelekea umoja huo kushindwa kujiendeleza.
Amesema uuzwaji holela wa maziwa mitaani unapelekea ushirika huo kudorola kutokana na wao kushindwa kujiendesha kutokana na kuwepo kwa kodi nyingi.
"Ushirika unakusanya Maziwa lita 200 kwa siku lakini mfanyabiashara wa maziwa ambaye halipi kodi yoyote anaweza kukusanya lita 1000 ambazo anauza bila kufuata taratibu na sheria za usindikaji, jambo ambalo linapelekea ushirika kudorola"
Mwenyekiti huyo alisema kuwa sheria za uuzaji wa maziwa yaliyosindikwa zikisimamiwa vizuri tasnia hiyo ya Maziwa itakua na wafugaji watanufaika pamoja na vyama vya ushirika vya maziwa vitakua kwa kasi.
Meneja Mradi wa Tanzania Milk processing Project (TMPP) kutoka HEIFER International, Mark Tsoxo, amesema shirika hilo limefikia kaya za wafugaji zipatazo 1,022,000, kwa kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora, na namna bora ya kutafuta masoko ya maziwa pamoja na umuhimu wa kuwa kwenye vyama vya ushirika.
Tsoxo alisema kuwa kuna vyama vya ushirika 119, na kwamba shirika hilo la Heifer Internationa limeviwezesha vyama 109 vya Ushirika ambavyo vimeweza kuongeza ukusanyaji wa maziwa kutoka lita 14,600 kwa siku hadi kufikia lita 16,7000.
Awali Katibu Mkuu Mifugo Bw.Tixon Nzunda alipata fursa ya kuvikabidhi (Canes 80) Vifaa vya kukusanyia na kutunzia Maziwa kwa vikundi vya Ushirika 14 na Vikundi Vidogo vidogo 6, ambapo Pikipiki moja ilikabidhiwa kwa kikundi cha MUARA FRESH MILK ambapo vifaa hivyo pamoja na Pikipiki vimetolewa Msaada na Shirika la Heifer International Tanzania kwa Vikundi hivyo.