SERIKALI, IFAD KUENDELEZA MIRADI YA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ambapo wamejadili kuhusu miradi inayotekelezwa kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi.
Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika leo Januari 16, 2026, Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameonesha kufurahishwa na ujio wa ujumbe huo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa IFAD nchini.
Amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuimarisha mazingira kuwa rafiki ili kuruhusu wawekezaji na sekta binafsi kushiriki katika kusukuma maendeleo ya wananchi.
Ujumbe huo wa IFAD umeongozwa na Mkurugenzi wa Nchi na Mwakilishi wake nchini Tanzania Bw. Seth Meng pamoja na Mratibu wa Mpango wa Nchi wa IFAD Bi. Jacqueline Machangu.
Majadiliano hayo yalijikita kujadili mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) na Mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayotekelezwa kati ya sekta ya mifugo na uvuvi