Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
RAIS SAMIA KUONGOZA MAWAZIRI ZAIDI YA 70 KUJADILI UCHUMI WA BULUU JIJINI DAR ES SALAAM
RAIS SAMIA KUONGOZA MAWAZIRI ZAIDI YA 70 KUJADILI UCHUMI WA BULUU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwaongoza Mawaziri zaidi ya 70 kutoka mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) kujadili masuala mbalimbali ya uchumi wa buluu na kuweka mkakati wa pamoja kuimarisha sekta ya uvuvi.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 2024 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Uvuvi, Bahari,na Maji ya Ndani kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki utakaofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 9-13, 2024.
Waziri Ulega amesema mkutano huo utafunguliwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Septemba 11 na umepangwa kufanyika sambamba na Kongamano la Kimataifa kuhusu Mikakati ya Uboreshaji wa Mnyororo wa Uzalishaji wa Vyakula vya Majini ulioandaliwa na Serikali, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (FAO).
“Lengo la mkutano huu unganishi, kwa maana ya Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa OACPS, ni kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya uvuvi katika nchi wanachama ikiwa ni pamoja na kuweka mkakati wa pamoja kuhusiana na sera zinazohusiana na masuala ya uvuvi na ufugaji viumbe maji ili kuimarisha sekta ya uvuvi katika kuchangia uchumi wa nchi wanachama. Pia, Mkutano huo utatumika kama Jukwaa jumuifu litakolokutanisha watunga sera na watalaamu wetu na wenzao kutoka mataifa wanachama ili kujadili fursa na changamoto zilizopo kwenye uchumi wa buluu na hatimae kujifunza mikakati ya kutatua changamoto hizo”, amesema
Ameongeza kuwa mkutano huo
pia utajumuisha Wataalam wa sekta ya uvuvi kutoka nchi wanachama na ulimwenguni kwa ujumla wake, Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali, Taasisi za Kikanda, Watafiti, Vyuo Vikuu, na Wavuvi Wadogo ambao ndiyo wahusika wakuu wa mkutano huo.
Kwa Mujibu wa Waziri Ulega mkutano huo utaleta nchini manufaa mengi ikiwemo Kufungua fursa za uwekezaji kwenye uchumi wa buluu hususan kwenye maeneo makuu mawili ya uvuvi na ufugaji samaki, kuendelea kuboresha mahusiano ya matumizi ya rasilimali za maji ya asili na zile za ukuzaji viumbe maji, baina ya wadau wetu wale wa mataifa wanachama.
Halikadhalika, kufungua wigo wa masoko ya nje ya mazao yetu ya uvuvi, kuongeza uwanda mpana wa wavuvi wetu kujifunza namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija, kujenga mahusiano mema kimataifa, na zaidi sana kuvutia uwekezaji kwenye eneo la uvuvi wa bahari kuu.
Mkutano huo utafanyika kwa siku tano mfululizo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere na utafungwa na Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.