​​PROF. SHEMDOE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA SHIRIKA LA JICA

Imewekwa: Thursday 08, February 2024

PROF. SHEMDOE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAAZI WA SHIRIKA LA JICA

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amekutana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi kujadiliana utekelezaji wa makubaliano ya kuendeleza mradi wa Afya Moja unaoangalia magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwenye Mifugo kwenda kwa binadamu ikiwepo Brucellosis na Kifua Kikuu (TB).

Prof. Shemdoe amekutana na Mwakilishi huyo Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma Januari 7, 2024.

Mradi huo unasimamiwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Maprofesa kutoka Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Maprofesa kutoka Chuo cha Mifugo cha Rakuna, kilichopo katika Mji wa Hokaido nchini Japan.

.