Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

DKT. KIJAJI AITAKA BODI YA TVLA KUSIMAMIA NIDHAMU ZA WATUMISHI

Imewekwa: 25 March, 2025
DKT. KIJAJI AITAKA BODI YA TVLA KUSIMAMIA NIDHAMU ZA WATUMISHI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameiagiza Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kusimamia nidhamu za  watumishi wote ambao hawatekelezi majukumu waliyopangiwa. 

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema Machi 21, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwenye ukumbi wa Wakala ulipo Temeke Jijini Dar es Salaam.

“Nisisitize kwa wajumbe wa Bodi, msisite kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi watakaothibitika kwenda kinyume na maelekezo ya Serikali pamoja na watakaotengeneza mazingira ya kupata chochote kwenye huduma ambayo aliiomba kuwahudumia Watanzania.”  

“Tufanye kazi kwa uadilifu na uaminifu mkub…
[11:35, 22/03/2025] Tanzania: DKT. KIJAJI AITAKA BODI YA TVLA KUSIMAMIA NIDHAMU ZA WATUMISHI 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameiagiza Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kusimamia nidhamu za  watumishi wote ambao hawatekelezi majukumu waliyopangiwa. 

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema Machi 21, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwenye ukumbi wa Wakala ulipo Temeke Jijini Dar es Salaam.

“Nisisitize kwa wajumbe wa Bodi, msisite kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi watakaothibitika kwenda kinyume na maelekezo ya Serikali pamoja na watakaotengeneza mazingira ya kupata chochote kwenye huduma ambayo aliiomba kuwahudumia Watanzania.”  

Mhe. Dkt. Kijaji ameongeza kwa kusisitiza uadilifu na uaminifu kwa watumishi wa Wakala hiyo na kuitaka taasisi hiyo kufanya udhibiti utakaowezesha uwekezaji wa kibiashara ili kuendana na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita.

Kuhusu Sekta ya Mifugo  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameitaka Bodi ya TVLA kuhakikisha inasimamia kwa ufanisi afya za mifugo nchini ambapo kuwa kituo cha umahiri kutoa bidhaa na  kufanya tafiti za  Magonjwa ya wanyama na wadudu waenezao  ndani na nje ya nchi.

Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte alisema Wizara ina Taasisi nyingi kwenye sekta ya Mifugo lakini TVLA ni Taasisi mama kwani inachangia kwa kiasi kikubwa sekta ya Mifugo isiyumbe kwa hiyo wizara kwa sasa inategemea uwepo wa Bodi uwe  na mchango mkubwa kwa maendeleo ya sekta ya Mifugo.

“Kwa uongozi wenu tunategemea Taasisi hii mbali na kushiriki kwenye zabuni hapa nchini iwe na uwezo wa kushiriki hata nje ya Tanzania, tuweze kuuza chanjo nje na kutoa huduma.” Alisema Ndg. Mhinte.

Naye  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TVLA, Prof. Amandus  Muhairwa amemshukuru Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kwa kuwaamini na kuwateua kushika dhamana ya kusimamia na kushauri maendeleo ya TVLA ambayo ni Taasisi muhimu katika uimarisaji wa afya za Mifugo nchini.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo