Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

DKT. BASHIRU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAONESHO YA MIFUGO

Imewekwa: 19 June, 2026
DKT. BASHIRU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAONESHO YA MIFUGO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameridhishwa na maandalizi kuelekea Maonesho na Mdana wa Mifugo 2026 yanayozikutanisha nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Namibia yatakayofanyika Ubena Zomozi, ambapo Maonesho hayo yanatarajiwa kuzinduliwa kesho tarehe 19 Juni, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Akizungumza leo Juni 18, 2026 Wilayani Chalinze Mkoani Pwani, wakati akikagua Maendeleo ya Maandalizi hayo, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema mpangilio wa Maonesho ya Mifugo umekaa vizuri, na amewapongeza wadau mbalimbali walioshiriki kuandaa Maonesho hayo ambayo yatafungua fursa kwa wafugaji nchini.

"Maonesho haya ni fursa kwa wafugaji kwani wataweza kujifunza jinsi ya kufuga kisasa na kwa tija, na kupata elimu mbalimbali kuhusu Malisho ya Mifugo" amesema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru 

Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameipongeza Menejimenti ya Wizara kwa Maandalizi mazuri ya Kilimo cha Malisho, ambapo amewataka Watendaji wa Wizara kutoa elimu ya kutosha kwa wafugaji kuhusu Malisho hayo na matumizi ya Teknolojia mpya ya ufugaji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo