ZAIDI YA MIFUGO MILIONI 70 KUCHWANJWA NCHI NZIMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amesema Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na utambuzi wa mifugo kwa mwaka 2024/2025 itakamilika mwezi agosti ambapo zaidi ya mifugo milioni 70 itachanjwa nchi nzima kukingwa dhidi ya magonjwa yanayoathiri biashara ya mifugo na mazao yake.
Bi. Meena amesema hayo Julai 5, 2025 wakati wa uhamasishaji wa kampeni ya Kitaifa ya Uchanjaji na Utambuzi wa mifugo katika katika kijiji cha Mpandangindo Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani ni Ruvuma ambapo amewahakikishia wafugaji wote nchini kuwa chanjo za mifugo ni salama kwa mifugo yote.
" Kampeni hii ni ya miaka mitano sahivi tunachanja na hadi mwezi agosti mwaka huu mpango huu utakuwa umekamilika ambapo tutakuwa tumechanja ng'ombe milioni 19, Mbuzi na Kondoo milioni 17 na Kuku milioni 40, chanjo zetu ni salama kwa ajili ya mifugo yetu" amesema Bi. Meena.
Aidha Katibu Mkuu Bi. Meena amewahimiza wafugaji wote nchini kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kwa kutoa mifugo yao kupata chanjo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo amesema mkoa huo utaendelea kumilikisha ardhi kwa wafugaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
" Sisi kama mkoa tutawamilikisha wafugaji maeneo kwa ajili ya malisho ikiwa ni hatua muhimu za kukabiliana na migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi." Alisema Jumanne.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Kanda ya Kusini (CCWT) Prisca Kaponda amemewahimiza wafugaji wote wa kanda huo kushirki kikamilifu Kampeni ya chanjo na Utambuzi wa Mifugo kwani Chanjo hizo ni salama kwa sababu zimezalishwa ndani ya nchi.