Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

WATUMISHI WAPYA WAPATIWA MAFUNZO

Imewekwa: 10 October, 2025
WATUMISHI WAPYA WAPATIWA MAFUNZO

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendesha Mafunzo kwa watumishi wapya wa Wizara hiyo yaliyofanyika  Oktoba 7, 2025 kwenye Ukumbi uliopo jengo la Wizara hiyo jijini Dodoma, lengo likiwa ni Kuwajengea uelewa kuhusu kazi zinazotekelezwa na Wizara hiyo pamoja na Kanuni , Sheria na Taratibu za Kiutumishi katika eneo lake la kazi.

Akiongoza mafunzo hayo Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu Dkt. Charles Mhina amewapongeza watumishi hao kwakupata nafasi yakuchaguliwa kutumikia Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuwataka washirikiane na kushikamana katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni za kiutumishi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo