Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

WAFUGAJI KATAVI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWENYE UCHANJAJI NA UTAMBUZI WA MIFUGO.

Imewekwa: 06 July, 2025
WAFUGAJI KATAVI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWENYE UCHANJAJI NA UTAMBUZI WA MIFUGO.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mhe. Shamimu Mwariko amewahimiza wafugaji wote kujitokeza katika zoezi la kampeni ya uchanjaji na utambuzi wa mifugo ili waweze kunufaika na zoezi hilo.

Ameyasema hayo Julai 4, 2025 wakati wa zoezi la utekelezaji wa kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo lililofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe mkoani katavi.

Aidha Mhe. Mwariko amesema zoezi hilo la chanjo na utambuzi wa mifugo litawasaidia watendaji kuweza kuandaa mpango bora utakao saidia kutoa huduma sahihi kwa wafugaji na kusimamia mifugo katika maeneo yao.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt. Pius Mwambene amesema kwa upande wa Mkoa wa katavi serikali inatarajia kuchanja Mifugo zaidi ya 800,000  ambapo zaidi ya Ng'ombe 200 wamesha patiwa chanjo na kutambuliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe.

Dkt Mwambene amesema serikali imetoa ruzuku kwenye chanjo ambapo kwa upande wa Ng'ombe serikali imechangia nusu bei shilingi 500 na kwa upande wa Mbuzi na Kindoo serikali imechangia nusu bei shilingi 300 pia upande wa kuku chanjo hiyo itatolewa bure na hereni zitatolewa bure.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo