TUTATEKELEZA MAONO YA RAIS SAMIA-DKT.BASHIRU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa juhudi ili kutekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya sekta hizo za uzalishaji.
Dkt. Kakurwa amesema hayo mara baada ya kupokelewa na Watumishi wa Wizara hiyo Novemba 18,2025 Wizarani hapo ikiwa ni muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo.
"Sote tumesikia aliyosema Mhe. Rais kupitia hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge kuhusu sekta zetu za Mifugo na Uvuvi hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunatekekeza maono hayo kwa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake kwa nafasi aliyonayo" Amesema Dkt. Bashiru.
Aidha Dkt. Bashiru amewataka watumishi hao kutoa ushirikiano wa kutosha kwake na Naibu Waziri Mhe. Ng'wasi Kamani katika kipindi chote cha kuwahudumia wananchi hususan wadau wa sekta za Mifugo na Uvuvi.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru na Naibu wake Mhe. Kamani waliteuliwa na Rais Samia kushika nyadhifa hizo Novemba 17,2025.