Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

SERIKALI YAELEZA MKAKATI WA WA KUENDELEZA MINADA YA MIFUGO

Imewekwa: 30 January, 2026
SERIKALI YAELEZA MKAKATI WA WA KUENDELEZA MINADA YA MIFUGO

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeeleza mkakati wa Serikali wa kuendeleza Mnada wa Mifugo wa Magena uliopo mpakani, kwa lengo la kukuza biashara ya mifugo na kurahisisha usafirishaji wa mifugo kwenda katika nchi jirani. 

Hayo yamesemwa Leo Januari 29,2026 Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Kamani , wakati akijibu la swali la mbunge wa Tarime Mjini Mhe. Esther Matiko,aliyetaka kujua  mkakati wa Serikali wa kuendeleza mnada wa Mifugo wa Magema, amesema Mnada wa Magena.

“Katika jitihada za kuendeleza mnada huo, serikali imeendelea kuboresha miundombinu muhimu ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022, kiasi cha shilingi milioni 175.65 kilitengwa na kutumika kujenga mazizi, kipakilio, birika la maji pamoja na vyoo, na miundombinu hiyo imekamilika.”Mhe. Kamani.

Aidha , amesema kuwa pamoja na uwepo wa miundombinu hiyo, Mnada wa Magena bado haufanyi vizuri kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo utoroshaji wa mifugo kwenda nchi jirani unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu, hali inayosababisha idadi ndogo ya mifugo kupelekwa kwenye mnada huo.

Amesema kuwa Ili kukabiliana na changamoto hizo na kuongeza mapato yatokanayo na biashara ya mifugo, Wizara yake  kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inaendelea kutoa elimu na kuhamasisha wadau kutumia mnada wa Magena kama ilivyokusudiwa wakati wa kuanzishwa kwake, sambamba na kuimarisha udhibiti wa utoroshaji wa mifugo.

Wakati huohuo ameongeza kuwa Serikali inahakikisha kuwa wakulima wazao la mwani wanapata tija kutokana na zao hilo kwa kuwapa elimu na kuwahamasisha kutengeneza vikundi Ili kuweza kupata soko Kwa uharaka.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo