Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

RAIS SAMIA ANATAKA TUFANYE MAAMUZI YANAYOTOKANA NA UTAFITI-DKT. BASHIRU

Imewekwa: 05 December, 2025
RAIS SAMIA ANATAKA TUFANYE MAAMUZI YANAYOTOKANA NA UTAFITI-DKT. BASHIRU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka viongozi na watendaji wa Serikali yake kufanya maamuzi yanayotokana na matokeo ya utafiti.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Disemba 05,2025 jijini Dar-es-salaam wakati akizungumza na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) alikofika akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Ng’wasi Kamani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Agnes Meena, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Edwin Mhede na baadhi ya watendaji wa Wizara   ambapo aliwataka wataalam hao kutambua umuhimu wa Taasisi hiyo kwa maslahi ya Taifa.

“Katika umuhimu wa Taasisi hii na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya 6 juu ya kukuza sekta hii ya Uvuvi ili iwe na mchango mkubwa kwenye uchumi wetu, nimetumwa na Mhe. Rais nifanye ziara ya kwanza kwenye kituo hiki ambapo anataka tufanye mambo yanayotokana na ushauri,tusifanye maamuzi kwa mihemko” Amesema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kituo hicho Mhe. Balozi Dkt. Bashiru na viongozi wengine alioambatana nao walielekea kwenye Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO).

Mrejesho, Malalamiko au Wazo