RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA, KWA WATOTO

Imewekwa: Friday 10, January 2025

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA, KWA WATOTO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametaka wazazi na walezi wa watoto kutekeleza vyema majukumu yao katika malezi ili shule ziwe na watoto wenye nidhamu na maadili kwa kuwaandaa kuwa wataalamu na viongozi.

Waziri Mhe. Dkt. Kijaji amesema hayo (09.01.2024) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya ujenzi ya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari za Nyerere, Semkiwa, Makorola, na Foroforo zilizopo Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

Amewakumbusha wazazi na walezi kufuata maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua jukumu la kulea watoto kwa kusimama katika nafasi zao ili shule zinazojengwa zipate watoto wenye nidhamu na malezi bora.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji anafanya ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Tanga ambapo tayari amefanya ziara ya siku mbili katika Wilaya ya Lushoto na sasa yupo katika Wilaya ya Korogwe akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi ya inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Tanga, kupitia kauli mbiu ya “Waone na Wasikie.”

.