WANANCHI WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Imewekwa: Friday 10, January 2025

WANANCHI WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo zilizofikishwa katika Wilaya ya Korogwe zimefanyiwa kazi kadri ilivyotarajiwa.

Akizungumza leo (09.01.2025) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magoma Makangara, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, amesema hayo mara baada ya baadhi ya wananchi kusema wameridhishwa na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Kijaji ametembelea, amekagua na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya ujenzi ya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari za Nyerere, Semkiwa, Makorola na Foroforo pamoja na ujenzi wa nyumba ya Afisa Ugani Kata ya Magoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji anafanya ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Tanga ambapo tayari amefanya ziara ya siku mbili katika Wilaya ya Lushoto na sasa yupo katika Wilaya ya Korogwe akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi ya inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Tanga, kupitia kauli mbiu ya “Waone na Wasikie.”

.