PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA NGURUWE AFRIKA, ATAJA FURSA ZA KIUCHUMI.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda amesema Kongamano la Nguruwe Afrika limelenga kuonesha fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa nguruwe, kukutanisha wadau, kubadilishana uzoefu na kukuza soko la Nguruwe pamoja na bidhaa zake kitaifa na Kimataifa.
Akifungua Kongamano hilo ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2025 Mhe. Pinda amesema Tanzania imepata fursa ya kipekee ya kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Ufugaji wa Nguruwe ambalo litaenda kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo katika tasnia ya nguruwe, kuongezea Wigo wa masoko ya Nguruwe na bidhaa zake katika nchi za Afrika.
" Tukio hili sio tu mkusanyiko wa wataalam, wakulima, wawekezaji na watunga sera bali ni sherehe ya sekta ambayo inabadilisha maisha ya wananchi katika taifa letu, kwa hiyo Tanzania imepata fursa ya kipekee ya kuongeza fursa ya mnyororo wa thamani wa nguruwe ", amesema Mhe. Pinda.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amesema serikali ya Tanzania imejipanga kuimarisha huduma za mifugo, utafiti na ushirikiano na sekta binafsi ili kuinua uzalishaji wa nguruwe nchini.
Bi Meena amesema Kongama hilo linawaleta wadau karibu pamoja na waadau mbalimbali lengo kubwa ikiwa na kukutana na kujadiliana kuhusiana na changamoto wanazokutanazo kwenye Ufugaji wa Nguruwe kwa ajili ya kuboresha na kuziondoa ikiwepo ugonjwa wa homa ya Nguruwe na changamoto ya masoko.
Aidha, Bi Meena ameongezea kwa kusema kupitia mkutano huu utawasaidia sana wakulima na wafugaji na wakitoka hapa wataweza kupata fursa za masoko kwa sababu inaleta kujuana na watu mbalimbali ndani na nje ya Nchi.
Pia, amesema Serikali kazi yake kubwa ni kutoa huduma na huduma kubwa ni ya kutoa tiba kwa maana ya tafiti mbalimbali na kuwezesha kuwaunganisha wafugaji wa ndani ya Nchi na nje ya Nchi pamoja na kuweza kupata masoko