MIFUGO NA UVUVI KUONGOZWA NA SAYANSI KUELEKEA DIRA 2050
SERIKALI imetaka Wataalamu wa Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau nchini kuimarisha matumizi ya sayansi, teknolojia, ubunifu na ujasiriamali ili kuongeza tija katika uzalishaji, kuboresha ubora wa bidhaa na kuimarisha minyororo ya thamani ya sekta hizo kuelekea utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, wakati akifungua Kongamano la 49 la Kitaaluma na Mkutano Mkuu wa 50 wa Chama cha Wataalamu Wazalishaji wa Wanyama wa Tanzania (TSAP), leo Oktoba 28, 2026 mkoani Iringa.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inalenga kuhakikisha nchi inafikia utoshelevu wa chakula, hususan protini inayotokana na mazao ya mifugo na uvuvi, yakiwemo nyama, maziwa, mayai na samaki ambapo amewasisitiza wataalamu wote wa mifugo nchini kutumia ipasavyo matokeo ya tafiti za kisayansi, kuendeleza ubunifu wa kiteknolojia na kutoa huduma zenye ubora ili kuongeza uzalishaji, kupunguza changamoto zinazowakabili wafugaji na wavuvi, pamoja na kuwezesha upatikanaji wa masoko bora, salama na ya uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.
Aidha,amesisitiza umuhimu wa kuzinlgatia maadili ya taaluma, uwajibikaji na ubora wa huduma, sambamba na kuimarisha afwya ya mifugo na samaki, upatikanaji wa malisho na chakula bora, pamoja na kuandaa mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Uzalishaji wa Wanyama Tanzania, Dkt. Zabron Nziku amesema kwa kipindi cha miaka 49, Chama hicho kimeendelea kuwaanganisha wataalam, watafiti, wahadhiri, wananfunzi na wakuu wa sekta za mifugo katika kukuza sayansi, teknolojia, wanasayansi, ubunifu na maendeleo endelevu ya uzalishaji wa mifugo kwa kuimarisha sera, tafiti, ugan, biashara na tija ambapo kwa sasa chama hicho kina jumla ya wanachama 1000.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Fabian Madele amesema wanataaluma hao watumie mkutano huo TSAP kubadilishana uzoefu, maarifa na namna ya kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kupitia taaluma zao, huku Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Benjamin Sitta akihimiza watalaam kufanya tafiti zinazotatua changamoto za wananchi.