Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MIFUGO 326,000 YACHANJWA NA KUTAMBULIWA

Imewekwa: 06 July, 2025
MIFUGO 326,000 YACHANJWA NA KUTAMBULIWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa takribani mifugo 326,000 imeshachanjwa na kutambuliwa tangu kuanza utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo Julai 02, 2025.

Mhe. Dkt. Kijaji amesema hayo Julai 05, 2025 Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu alikofika kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa kampeni hiyo ambapo amebainisha kuwa hatua hiyo inatoa ujumbe kwa jumuiya za kimataifa kuendelea kufungua masoko ya mifugo hai na mazao yake kutoka hapa nchini.

“Tupo tayari kuongeza thamani ya Mifugo yetu kwa sababu Mhe. Rais alishatuletea mbegu bora za madume ya Ng’ombe 754 ambao wameshasambazwa kwa wafugaji kote nchini na sasa tunaenda kuchanja mifugo yetu huku pia Mhe. Rais Samia akisikiliza kilio cha wafugaji kwa kuwaondolea gharama ya kutambua mifugo yao kwa kutumia hereni za kielektroniki” Ameongeza Mhe. Dkt. Kijaji 

Akielezea namna kampeni hiyo itakavyowasaidia kuongeza thamani ya Nyama wanayosindika kwenye kiwanda chao Mkurugenzi wa kiwanda cha “Union Meat” amesema kuwa Chanjo na Utambuzi wa Mifugo itasaidia kuongeza imani ya bidhaa hiyo kwenye soko la kimataifa.

“Mimi nilikuwa Jaji nchini Ushelisheli lakini baada ya kuona namna mazingira rafiki ya uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo aliyoweka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliamua kurudi nchini na kufanya uwekezaji na kupitia hii kampeni ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo yetu tayari thamani ya nyama tunayosindika imeongezeka” Amesema Bi. Ng’hwani.

Ziara hiyo ya Mhe. Dkt. Kijaji iliyolenga kukagua utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo iliyozinduliwa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Juni 16, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea katika mikoa ya Geita, Pwani, Morogoro, Tabora na Dodom

Mrejesho, Malalamiko au Wazo