Mhe. Waziri wa mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia paredi ya mifugo Mkoani Arusha

Posted On: Monday 13, August 2018

YALIYOJIRI KATIKA UZINDUZI WA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI KATIKA VIWANJA VYA THEMI - ARUSHA.
Mgeni rasmi katika ufunguzi alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli za mbalimbali za maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Themi - Arusha tarehe 05/08/2018
#Nimetembelea mabanda na kujionea shughuli mbalimbali, nawapongeza sana kwa kazi nzuri, nimefurahishwa na maonesho kutoka Halmashauri na mashamba darasa, Alisema - Mpina

#Vlevile kwa ufugaji bora mnaofanya , nimeona kwenye (paredi) kuna ng'ombe wanaotoa hadi lita 28, hongereni kwa kazi nzurii , Alisema - Waziri
#Kauli mbiu yetu ya leo ni "Wekeza katika Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa maendeleo ya viwanda" tukae tujiulize tunawekeza nini katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na tunachangamoto zipi, Alieleza - Waziri
#Aidha, kati ya ng'ombe mil 30 .5, ng'ombe mil 4 na laki 4 zote zinatoka ukanda wa kaskazini ambapo ni zaidi ya asilimia 10 ya ng'ombe wanatoka ukanda huu, Alieleza - Mpina
#Pia kati ya Kondoo mil. 5.3 kondoo mil 2.7 wanazalishwa Ukanda wa kaskazini, na Kati ya mbuzi Mil 18. 8 wanaozalishwa hapa ni mbuzi mil 4.1, Aliongezea kusema - Mpina.
#Kwapande wa uvuvi mna maeneo mengi ya maziwa na mabwawa, kwahiyo mnayo fursa nyingi za kufuga samaki na kupata vifaranga bora vya samaki. Alisema - Mpina
#Niwahakikishie kituo chenu cha Tanga kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 tutakiboresha na kukiimarisha vizur ili kiweze kuzalisha vifaranga bora vya samaki. Alisisitiza - Mpina
#Halmashauri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wote , Tokomezeni uvuvi haramu kwenye maziwa na mabwawa yetu, Kwanini tuagize samaki kutoka nje wakati tunaacha rasilkmali zetu zinafanyiwa uvuvi haramu. Alisema - Luhaga
#Ningeomba uzalishaji wa samaki uongezeke kama kuna soko la uhakika kwenye mazao haya inabidi tuwekeze vyakutosha, hatuzuii kuagiza nje lakini tuagize bidhaa zile tu ambazo hatuwez kuzalisha Nchini . - Mpina
#Wito wangu kwenu wekezeni katika Kilimo, Mifugo, na Uvuvi,pia muanzishe mashamba na mabwa makubwa ya kufuga samaki.
#Watendaji wangu kutoka Wizarani zungukeni maeneo yote ya wananchi na kuhamasisha ufugaji wa bora.
#Awali ya yote hakikisheni Kanda ya kaskazini kuna kuwa na viwanda vikubwa kuchinjia, kuchakata na kusindika nyama.
#Nataka wakenya waje kununua hapa nyama Watanzania wengi hatunufaiki mifugo mingi inatoroshwa ambapo Mbuzi laki 125 na ng'ombe 37 wametoroshwa kwenda nje ya Nchi.
#Wito wangu kwa Watendaji na Halmashauri zote ni lazma tupate kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, hatuna kiwanda kikubwa cha Usindikaji wa nyama, -
#Nawapongeza Halmashauri kwa kutenga maeneo elf 66, Nimuhimu kuendelea kutenga maeneo ya mifugo na tutakuja kuyatambua na kuyasajili, Alisema - Mpina
#Majosho hayafanyi kazi yote na mengine hayana miundo mbinu muhimu na machinjio hayafanyi kazi, pia Kituo chetu NAIC - Usa River kitaboreshwa zaidi na mapungufu yatatatuliwa. - Mpina
#Migogoro ya na Wakulima na Wafugaji lazma itatulike, migogor isiyokuwa na lazima haiitajiki, kila mtu aweze kuheshimu mifugo ya mwenzake, Alisistiza - Mpina
#Ni lazima tujipange na tuhakikishe Halmashauri wametenga maeneo ya mifugo, tutafatilia mimi na watendaji wangu kuhakikisha maeneo yaliyosemwa yametengwa - Mpina
#Natoa Maelekezo 6 kupitia ugeni wangu:-
1. Ninampa siku 7 Katibu Mkuu Kilimo kunieleza kwanini bei za mahindi na mtama zinazaliwa hapa mchini na zinauzwa kwa bei kubwa
2. Ninatoa siku 7 kwa Katibu Mkuu Mifugo nipate maelezo kwanini Bei ya Uhimilishaji inayotozwa ni kubwa wakati kituo ni cha serikali na mbengu zimahifadhiwa katika sehemu ya serikali.
3.Taasisi zinazohusika na Udhibiti wa madawa hapa nchini TPRI, TFDA na DVS wafanye tathmini ya utendaji wao wa kazi, kasoro zao kwanini wananchi wanunue dawa ambazo hazina ubora na wakati Taasisi hizo zipo.
4. Natoa miez 5 Halmashauri kuhakikisha majosho na mabwawa yanakaratibiwa na yanafanya kazi mwez wa 1 tarehe 1 mwakani, nikikagua nikakuta hakuna miundo mbinu muhimu nitafuta ukusanyaji wa kodi yoyote katika eneo lolote na makusanyo.
5. Pia Kila Halmashauri ziwe na mashamba darasa la malisho .. na kuhakikisha wananchi wanajifunza ufugaji wa samaki na Shamba la kuzalisha vifaranga vya samaki, kufikia June 2019 tujiridhishe kila Halmashauri lina bwawa la mfano. - Mpina
6.Mpango wa kudhbiti uvuvi haramu, wizara yangu imejipanga vizuri kushirikiana na watendaji wengine kuhakikisha uvuvi haramu wa kwenye mabwa, maziwa na mito yote yanakwisha - Waziri.
#Halmshauri wekeni mipango dhabiti ya kupambana na uvuvi haramu katika sehemu zote za maziwa,mito na mabwawa.
#Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano hakikisha katika viwanja vyetu vya ndege na bandari lazima kuwe na miundo mbinu bora na sehemu za kutunzia samaki na nyama zijengwe. - Mpina

.