Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MAFANIKIO YA MIAKA 4 YA SERIKALI YA AWAMU YA 6 KWENYE SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Imewekwa: 12 May, 2025
MAFANIKIO YA MIAKA 4 YA SERIKALI YA AWAMU YA 6 KWENYE SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI
*Migogoro ya wakulima na wafugaji nchini imepungua sana kwa kipindi cha miaka 4 hii ni kutokana na serikali kutenga maeneo ya kutosha ya malisho ya mifugo. *Wavuvi wamewezeshwa mitaji na vifaa lengo waweze kutekeleza wajibu wao vizuri ambapo mikopo ya Tshs Bil 397.8 imetolewa kwa mwaka 2025. *Vizimba 222 vimejengwa na kugawiwa kwa wafugaji samaki kwenye maji ya asili lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa samaki. *Ndege nyuki moja imenunuliwa kwa lengo la kuwabaini wavuvi haramu, ndege hii ina uwezo wa kukaa angani kwa saa mbili. *Boti za uvuvi 219 zimenunuliwa na kugawanywa maeneo mbalimbali. *Serikali inaendelea na mchakato wa kukamilisha ununuzi wa meli 8 za uvuvi *Ukuzaji wa viumbe maji (Samaki, Mwani, Jongoo bahari, vipande vya lulu) umeongezeka kutoka Tani 44,735 mwaka 2021 mpaka Tani 124,000 Mwaka 2025. *Uzalishaji wa vifaranga vya samaki umeongezeka kutoka 24,204,514 Mwaka 2021 hadi kufikia 110,771,956 Mwaka 2025. *Mialo 7 inaendelea kujengwa katika maeneo tofauti tofauti nchini. *Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko wafikia 81.9% na inatarajiwa kukamilika 30 Juni 2025. Watanzania 570 wamepata ajira za kudumu kwenye bandari hii. *Vijana 235 wamewezeshwa kupata mafunzo ya unenepeshaji wa mifugo kupitia mradi wa BBT. *Pikipiki 2,253 zimegawiwa kwa maafisa ugani ili kurahisisha zoezi la kuwafikia wafugaji katika jamii. *Zaidi ya Tshs Bil 267 zimetolewa kama mkopo kwa wafugaji wadogo wadogo. *Minada ya mifugo 51 imeboreshwa. Vituo 10 vya kukusanyia maziwa vimejengwa. *Katika kipindi cha miaka minne, Tani 13,745 za nyama zimeuzwa nje ya nchi kutoka Tani 1,774 Mwaka 2021. *Serikali imekuja na mpango mahsusi wa chanjo na utambuzi wa mifugo lengo likiwa ni kukidhi matakwa ya soko la kimataifa linalotaka kila mnyama awe amechanjwa na kuiwezesha serikali na wadau kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo yanayohusu sekta ya mifugo. *Chanjo zinazotolewaa na serikali ni salama kabisa kwani zimezalishwa na wazawa hapa hapa nchini hivyo wananchi wajitokeze kuchanja mifugo yao. *Serikali itaendelea kupambana na uvuvi haramu ili kulinda rasilimali za bahari, mito na maziwa. *Wizara inaendelea na zoezi la kung'oa na kuondoa magugu maji yaliyojitokeza Ziwa Victoria ili shughuli za uchumi ziweze kuendelea. * Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi imejipanga kuboresha na kulinda rasilimali za uvuvi na ufugaji kwani uvuvi na ufugaji ni hazina na utajiri wetu, hivyo unatakiwa kulindwa vyema.
Mrejesho, Malalamiko au Wazo