Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
KIWANDA CHATAKIWA KUANZA UZALISHAJI, KUFUATIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

KIWANDA CHATAKIWA KUANZA UZALISHAJI, KUFUATIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Edwin Mhede ameutaka uongozi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya uvuvi cha LIFA Products ltd, kilichopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza uzalishaji hivi karibuni.
Dkt. Mhede amebainisha hayo Machi 20, 2025 alipotembelea kiwanda hicho kujionea ujenzi na marekebisho kadhaa yanayofanywa kabla ya kuanza rasmi kwa uzalishaji wa kuchakata mazao ya uvuvi, huku akijulishwa baadhi ya nyaraka muhimu tayari zimekamilishwa na serikali.
Amesema serikali inaudai uongozi wa kiwanda hicho kwa kutoanza uzalishaji ilhali serikali imewawekea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kuhakikisha nyaraka muhimu kukamilishwa na kupatiwa miongozo kadhaa kutoka kwa wataalamu kutoka ngazi ya kata hadi taifa.
“Lazima tufanye kazi kiwanda hiki kianze kuzalisha na kianze kusafirisha bidhaa huko duniani, tunataka tuone kitu kinafanyika hapa na kama kuna eneo lingine lolote ambalo linamkwamo serikali ya mkoa ipo, sisi tupo na wataalamu wangu wilayani, mkoani hadi taifa tupo.” Amesema Dkt. Mhede
Aidha, amewataka wataalamu kutoka wizarani kufika katika kiwanda hicho mara kwa mara ili kuusaidia uongozi wa kiwanda kuhakikisha wanatoa bidhaa bora mara watakapoanza uzalishaji.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bw. Juma Chikoka amesema anataka kuona uzalishaji kwa kuwa serikali imeendelea kurahisisha na kuwajengea mazingira mazuri wawekezaji.
“Kiongozi hapa amefika, amerudi tena, maana yake dhamira yake na serikali ni njema, tusiangushe tena hili jambo, maana yake hili jambo likianguka Musoma na serikali ya wilaya tupo, mimi siyo muumini wa kuanguka.” Amesema Bw. Chikoka.
Pia, ameahidi kurudi katika kiwanda hicho Mwezi Aprili mwaka huu ili kujionea maendeleo ya kiwanda na kupata taarifa rasmi ya kuanza kwa uzalishaji wa kuchakata mazao ya uvuvi, hivyo kukamilisha mapema masuala ya kitaalamu.
Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha LIFA Products ltd. Bw. Mwita Masumbo amekiri kuwa kiwanda hicho kinadaiwa na serikali kwa kutoanza uzalishaji licha ya kukabidhiwa nyaraka muhimu zinazowaruhusu kuanza kuchakata mazao ya uvuvi.
Amesema uongozi wa kiwanda utafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kiwanda kinaanza uzalishaji hivi karibuni.