Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

DKT. MHEDE AONGOZA KIKAO CHA UHIFADHI WA BAHARI

Imewekwa: 26 September, 2025
DKT. MHEDE AONGOZA KIKAO CHA UHIFADHI WA BAHARI

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhede ameshiriki na kuongoza kikao kazi cha usimamizi wa mradi wa Tuhifadhi Bahari yetu kwa lengo la kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi huo

Mashirika yaliyoshiriki katika uwasilishaji wa Taarifa hiyo ni pamoja na Shirika la Umoja wa kimataifa kwa ajili ya Uhifadhi wa hali na Maliasili (IUCN), Mfuko wa Mazingira Ulimwenguni (WWF), Shirika la Uhifadhi wa Viumbe Asili (TNC), Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS) na FORUMCC

Aidha baada ya mashirika hayo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo Kamati inayosimamia mradi huo imeelekeza Wadau kushirikisha mamlaka za Serikali za mitaa, kuandaa majukwaa ya Vikundi vya usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi BMU’s, Kuhakikisha mpango kazi wa mradi unaendana na vipaumbele vya Wizara pamoja na Kuimarisha njia za utoaji taarifa

Mradi huo unalenga kuhifadhi mazingira ya Pwani na baharini kwa kuzingatia ajenda ya Uchumi wa Buluu

Mrejesho, Malalamiko au Wazo