Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

DKT. MADELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATAALAM KUTOKA MAURITIUS KUHUSU MIFUMO YA HUDUMA ZA MIFUGO

Imewekwa: 17 September, 2026
DKT. MADELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATAALAM KUTOKA MAURITIUS KUHUSU MIFUMO YA HUDUMA ZA MIFUGO

Naibu Katibu Mkuu wa Mifugo Dkt. Fabian Madele  leo Septemba 15, 2026  amepokea timu ya wataalam kutoka Jamhuri ya Mauritius  iliyoongozwa na Chief Veterinary Officer, Dkt. Beeharry Pitambarsing, na Senior Epidemiologist, Dkt. Bhishnee Devi Mungur, katika kikao kilochofanyika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Wataalam hao wamefika nchini kufanya uchambuzi wa utendaji wa mifumo ya huduma za mifugo  pamoja na kutathmini uwezekano wa kusafirishwa kwa vimelea vya magonjwa kupitia biashara ya mifugo na mazao yake kwenda Mauritius.

 Timu hiyo itakuwa nchini hadi Septemba 18, 2026 ambapo watatembelea maeneo mbalimbali yanayohusiana na huduma za mifugo na usalama wa biashara ya mifugo, yakiwemo Eneo la Kupumzisha Mifugo Kizoto, Kituo cha Karantini cha Alyakeen, Tanga, Bandari ya Tanga, Machinjio ya UMAL, Mashamba mawili yanayouza mifugo kwa ajili ya Machinjio ya UMAL na Maabara Kuu ya Mifugo (TVLA).

 Ziara hiyo inalenga kupata uelewa wa kina kuhusu mifumo ya udhibiti wa magonjwa, ukaguzi na uthibitishaji wa mifugo na mazao yake, pamoja na kuweka mazingira salama na yenye kuaminika kwa biashara ya mifugo kati ya Tanzania na Mauritius.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo