Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
DKT KIJAJI: "MAPINDUZI SEKTA YA MIFUGO YANAANZA NA MFUGAJI MWENYEWE”

DKT. KIJAJI: "MAPINDUZI SEKTA YA MIFUGO YANAANZA NA MFUGAJI MWENYEWE”
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuelekea mapinduzi makubwa katika Sekta ya Mifugo, miongoni mwa mambo muhimu ni wafugaji kuogesha mifugo yao ili kuwa bora na sekta hiyo kuchangia zaidi katika pato la taifa.
Mhe. Dkt. Kijaji amebainisha hayo leo (11.01.2025) wakati alipokuwa akizindua josho la kuogesha mifugo lililopo Kijiji cha Elerai Kata ya Kibirashi, Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga, ambapo amesema serikali itaendelea kujenga majosho ili kuhakikisha mifugo inakuwa bora dhidi ya magonjwa.
Amebainisha kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha ifikapo Mwaka 2030 mchango wa Sekta ya Mifugo katika pato la taifa kufikia zaidi ya asilimia 10 kwa kuwa na mifugo bora ambayo itatoa mazao bora na kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi kwa bei yenye tija kwa wafugaji na nchi kwa ujumla.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji anahitimisha ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Tanga ambapo leo hii yupo Wilayani Kilindi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Tanga, kupitia kauli mbiu ya “Waone na Wasikie.”