Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

BI. AGNES MEENA ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI WA MIFUGO SENEGAL

Imewekwa: 06 September, 2025
BI. AGNES MEENA ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI WA MIFUGO SENEGAL

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena ameshiriki katika Kikao cha  Mawaziri wa Mifugo kinachojulikana kwa jina la  'Livestock Ministerial Deep Dive'.
 
Majadiliano hayo ambayo yamefanyika leo Septemba 4, 2025 ni sehemu ya mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika unaofanyika , jijini Dakar nchini Senegal.

Kikao hicho kimelenga  kujadili vipaumbele, changamoto na suluhu za sekta ya mifugo kwa nchi za Afrika na kubainisha namna nchi hizo zinavyoweza kushirikiana katika  kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo. 

Katika mchango wake, Bi.  Meena amelezea vipaumbele  vya Tanzania kwa Sekta ya Mifugo na mikakati inayotekelezwa na  Serikali pamoja na matokeo yaliyopatikana. 

Aidha, alibainisha maeneo ya ushirikiano na wadau wa maendeleo, akisisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza mageuzi ya sekta ya mifugo kama sehemu ya nguzo ya Mifumo ya Chakula na maendeleo endelevu barani Afrika.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo