Albamu ya Video

 • MAABARA ZA KISASA ZA UTAFITI ZAZINDULIWA LITA TENGERU

  MAABARA ZA KISASA ZA UTAFITI ZAZINDULIWA LITA TENGERU

  December 03, 2020

  Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) kwa kushirikiana na serikali ya Poland imefanya ukarabati na kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya maabara mbili za utafiti wa magonjwa ya mifugo nchini.

 • WAFUGAJI KUSHIRIKISHWA KWENYE MIRADI, HUFANYA MIRADI HIYO KUDUMU.

  WAFUGAJI KUSHIRIKISHWA KWENYE MIRADI, HUFANYA MIRADI HIYO KUDUMU.

  December 01, 2020

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugp na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wafugaji wanaposhirikishwa katika uchangiaji wa miradi mbalimbali kwa ajili ya mifugo yao wamekuwa wakionyesha utayari na kufanya miradi hiyo kudumu kwa kuwa wanajisikia kuwa sehemu miundombinu hiyo. Akizungumza (30.11.2020) katika bwawa la kunyweshea mifugo maji la Elwaniolera lililopo kijiji cha Eluwai, Kata ya Monduli Juu, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Prof. Gabriel amesema wakazi katika eneo hilo wameonesha utayari wa kulifanyia ukarabati bwawa hilo linalohudumia zaidi ya wafugaji 2,000 katika vijiji vya Eluwai, Emairete na Enguiki kutokana na kina cha bwawa hilo kupungua kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo ya kilimo.

 • SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI NCHINI

  SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI NCHINI

  December 01, 2020

  Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo katika mchakato wa kukamilisha Mpango kabambe wa miaka 15 ijayo kuanzia 2021 utakaosimamia sekta ya Uvuvi na kutoa dira ya kulinda rasilimali za uvuvi ili sekta hiyo iweze kutoa mchango mkubwa na endelevu katika pato la taifa.

 • HAFLA YA KUKABIDHI INJINI KWA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAVUVI KANDA YA ZIWA VICTORIA.

  HAFLA YA KUKABIDHI INJINI KWA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAVUVI KANDA YA ZIWA VICTORIA.

  December 01, 2020

  Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah amekabidhi injini nne (4) za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi kanda ya Ziwa Victoria.

 • WAFUGAJI NA WAKULIMA KUNUFAIKA KUPITIA KIWANDA CHA NGURU HILLS

  WAFUGAJI NA WAKULIMA KUNUFAIKA KUPITIA KIWANDA CHA NGURU HILLS

  November 30, 2020

  Serikali imesema katika kuboresha na kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini ukiwemo Mkoa wa Morogoro, inasisitiza uwepo wa miradi ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa makundi yote mawili. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema hayo (28.11.2020) katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro alipotembelea ujenzi wa mradi wa kiwanda cha nyama katika Ranchi ya Nguru Hills na kubainisha kuwa mradi huo unaotarajia kukamilika mwezi Aprili Mwaka 2021 utakuwa na manufaa makubwa kwa wafugaji na wakazi wa Mkoa wa Morogoro.

.