Albamu ya Video

 • "Kafanyeni kazi kwa ufanisi na muhakikishe mnakusanya mapato." Prof. Gabriel

  June 10, 2020

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel 05.02.2020 amefungua kikao cha kupitia taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa maafisa kutoka vituo vya mifugo (ZVC), minada ya upili na mipakani na maeneo ya mikakati. Kikao hicho kimefanyika kwa siku mbili katika ofisi za wizara hiyo zilizopo katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma.

 • KIPINDI: MIFUGO NA UVUVI (JITIHADA ZA SERIKALI KUFUFUA TAFICO)

  KIPINDI: MIFUGO NA UVUVI (JITIHADA ZA SERIKALI KUFUFUA TAFICO)

  June 10, 2020

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaandaa mfululizo wa vipindi vya redio na televisheni ambavyo lengo lake kuu ni kutoa elimu na kukufahamisha majukumu ya wizara ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kwa mwananchi na taifa kwa ujumla. Katika kipindi hiki utafahamu jitihada za serikali kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) na namna Serikali ya Tanzania ilivyopata msaada wa Shilingi Bilioni 4.2 kutoka Serikali ya Japan ili kufufua shirika hilo.

 • Mifugo 578 iliyokamtwa katika msitu wa Tongwe Mashariki, Waachiwa

  Mifugo 578 iliyokamtwa katika msitu wa Tongwe Mashariki, Waachiwa

  June 10, 2020

  Wilaya ya Tanganyika, Tarehe 28/01/2019: Wafugaji waliongiza mifugo zaidi ya 570 na kushikiliwa ndani ya hifadhi walipa faini ya papo kwa papo ya Mil 11.4 badala ya faini iliyokuwa imetozwa awali ya Mil. 60 ambayo ni kinyume na Sheria ya Hifadhi ya Misitu Na.14 ya mwaka 2002, Serikali imetafakari na kuridhia walipe faini hiyo.

 • Ni lazima tuanze kutumia mizani- Prof. Ole Gabriel

  Ni lazima tuanze kutumia mizani- Prof. Ole Gabriel

  June 10, 2020

  Ni kwenye minada yote ya mifugo hapa nchini.

 • Waziri Mpina atangaza kampeni ya Kitaifa ya uzalishaji Kuku nchini

  Waziri Mpina atangaza kampeni ya Kitaifa ya uzalishaji Kuku nchini

  June 10, 2020

  Tunahitaji kuku wengi tuliuzie Bara la Afrika na Dunia. - PWANI

.