Albamu ya Video

 • YALIYOJIRI MWEZI JANUARI 2020

  YALIYOJIRI MWEZI JANUARI 2020

  June 17, 2020

  Karibu mtazamaji wa mifugouvuvi Online Tv katika kipindi hiki cha "Yaliyojiri" ambapo kitakuwa kinakukusanyia baadhi ya matukio muhimu ambayo yamefanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi yanayoshirikisha viongozi, taasisi na idara zilizo chini ya wizara hii. Katika kipindi ungana na Afisa Habari wa wizara hii Omary Mtamike ambaye anakufahamisha baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri kwa Mwezi Januari Mwaka 2020.

 • Wadau wakieleza faida ya mafunzo ya ufugaji bora

  Wadau wakieleza faida ya mafunzo ya ufugaji bora

  June 17, 2020

  Wadau wakieleza faida ya mafunzo ya ufugaji bora

 • "Tumejadiliana uwekezaji katika sekta ya uvuvi." Bw. Bulayi

  June 10, 2020

  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bw. Emmanuel Bulayi amefanya mazungumzo na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya (AfDB) ukiongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya sekta za kilimo na Maendeleo Vijijini Bi. Toda Atsuko, Mkurugenzi Mkaazi wa benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru pamoja na maafisa wengine kutoka katika benki hiyo. Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma (06.02.2020) kimehudhuriwa pia na maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi

 • "Wizara inataka uwekezaji utakaoinua uchumi wa wafugaji." Katibu Mkuu Prof. Gabriel

  June 10, 2020

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masuala ya Sekta za Kilimo na Maendeleo Vijijini kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bi. Toda Atsuko pamoja na maafisa wengine kutoka katika benki hiyo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, akisisitiza uwekezaji wa benki hiyo katika sekta ya mifugo ili kuinua uchumi wa wafugaji. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma. (05.02.2020)

 • KIPINDI: MIFUGO NA UVUVI (NAMNA MALIGHAFI ZA MIFUGO ZINAVYOONGEZEWA THAMANI)

  KIPINDI: MIFUGO NA UVUVI (NAMNA MALIGHAFI ZA MIFUGO ZINAVYOONGEZEWA THAMANI)

  June 10, 2020

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaandaa mfululizo wa vipindi vya redio na televisheni ambavyo lengo lake kuu ni kutoa elimu na kukufahamisha majukumu ya wizara ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kwa mwananchi na taifa kwa ujumla. Katika kipindi hiki utafahamu namna malighafi za mifugo zinavyoongezewa thamani kupitia viwanda vilivyopo hapa nchini kikiwemo kiwanda cha 'Happy Sausage' ambacho kinachomilikiwa na mtanzania.

.