Albamu ya Video

 • YALIYOJIRI MACHI, 2021!

  YALIYOJIRI MACHI, 2021!

  September 20, 2021

  Tazama matukio yaliyojiri ndani ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mwezi Machi, 2021.

 • KIPINDI: UMUHIMU WA SHAMBA LA NGERENGERE KWA WAFUGAJI NCHINI

  KIPINDI: UMUHIMU WA SHAMBA LA NGERENGERE KWA WAFUGAJI NCHINI

  September 20, 2021

  Shamba la Mifugo la Ngerengere lililopo mkoani Morogoro ni miongoni mwa mashamba ambayo yamekuwa yakitoa mchango Mkubwa kwa wafugaji hapa nchini ambapo mbali na kutoa mbegu bora za mifugo, wataalam wake wamekuwa wakitoa elimu kwa wafugaji wanaolizunguka.... Tazama zaidi hapo

 • WAZIRI NDAKI ASISITIZA MATOKEO CHANYA KATIKA BAJETI 2021/2022

  WAZIRI NDAKI ASISITIZA MATOKEO CHANYA KATIKA BAJETI 2021/2022

  September 20, 2021

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi yawasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/21 na makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 (29.03.2021)

 • MASHAMBA DARASA YA UFUGAJI SAMAKI KUANZISHWA KOTE NCHINI

  MASHAMBA DARASA YA UFUGAJI SAMAKI KUANZISHWA KOTE NCHINI

  September 20, 2021

  Serikali imesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 ina mpango wa kuanzisha vituo vya ukuzaji viumbe maji katika halmashauri 80 za wilaya ikiwa na lengo la kuhakikisha kila halmashauri inakuwa na kituo hicho ambacho kitatumika kama shamba darasa kwa ajili ya kufundisha wananchi namna ya kufuga samaki. Akizungumza (17.03.2021) wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kituo cha ukuzaji viumbe maji kinachozalisha vifaranga vya samaki cha Kingolwira kilichopo Mkoani Morogoro, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amesema mkakati wa serikali kupitia vituo hivyo vitakavyokuwepo katika halshamauri zote za wilaya ni kuwa na samaki wengi wafugwao kwa njia mbalimbali ikiwemo ya mabwawa na kufikia uzalishaji wa samaki wa asilimia 50 kwa njia ya kufuga na asilimia 50 wanaotokana na maji ya asili.

 • NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. PAULINE GEKUL AMEYASEMA HAYA ALIPOTEMBELEA MNADA WA KIZOTA.

  NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. PAULINE GEKUL AMEYASEMA HAYA ALIPOTEMBELEA MNADA WA KIZOTA.

  September 20, 2021

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul amewataka wafanyabiashara wanaotunza mifugo yao katika mnada wa Kizota ikisubiri kuchinjwa kuiondoa mifugo hiyo ndani ya siku 5.

.