Albamu ya Video

 • WIZARA KUJENGA VITUO 40 VYA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI, UHOLANZI YAVUTIWA!

  WIZARA KUJENGA VITUO 40 VYA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI, UHOLANZI YAVUTIWA!

  September 20, 2021

  Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jeroen Verheu amesema nchi yake iko tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya mafunzo ya ufugaji samaki nchini ili kuunga mkono mkakati wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inafikisha huduma za mafunzo hayo kila wilaya. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza jana (10.04.2021), mara baada ya kufanya mazungumzo na balozi huyo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam, amesema Mhe. Balozi Verheu ameridhishwa na mkakati wa wizara ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo arobaini vya mafunzo ya ufugaji samaki.

 • WACHUNAJI MANISPAA YA TABORA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MBINU BORA ZA UCHUNAJI NGOZI

  WACHUNAJI MANISPAA YA TABORA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MBINU BORA ZA UCHUNAJI NGOZI

  September 20, 2021

  WACHUNAJI KATIKA MACHINJIO YA MANISPAA YA TABORA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MBINU BORA ZA UCHUNAJI NGOZI NA MATUMIZI YA VIFAA STAHIKI.

 • PROF. GABRIEL ASISITIZA MATUMIZI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOA TAARIFA ZA SHUGHULI ZA SERIKALI.

  PROF. GABRIEL ASISITIZA MATUMIZI YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOA TAARIFA ZA SHUGHULI ZA SERIKALI.

  September 20, 2021

  Prof. Ole Gabriel asisitiza matumizi ya vyombo vya habari katika kuhabarisha Umma kuhusu shughuli mbalimbali za Serikali.

 • WAZIRI NDAKI AJIBU MASWALI BUNGENI KWA MARA YA KWANZA!

  WAZIRI NDAKI AJIBU MASWALI BUNGENI KWA MARA YA KWANZA!

  September 20, 2021

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akijibu maswali katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo.

 • Waziri Ndaki Amtumbua Ofisa Msimamizi Wa Mnada Igunga

  Waziri Ndaki Amtumbua Ofisa Msimamizi Wa Mnada Igunga

  September 20, 2021

  WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amemsimamisha kazi Ofisa anayesimamia Mnada wa Mifugo wa Upili ulioko Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Bw. Juma Athuman kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mapato. Mhe. Ndaki amechukua hatua hiyo juzi alipotembelea mnada huo ili kuangalia ufanisi wake ambapo alibaini kutokuwepo nyaraka za kumbukumbu ya mifugo inayoingia na kutoka katika mnada huo kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

.