Albamu ya Video

 • TZ 9+ WAFUGAJI WATAKIWA KUYASIMAMIA NA KUYATUNZA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MIFUGO

  TZ 9+ WAFUGAJI WATAKIWA KUYASIMAMIA NA KUYATUNZA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MIFUGO

  September 20, 2021

  Mhe. Ndaki awasihi wafugaji kumiliki ardhi kwa ajili ya kupata maeneo ya malisho na kuhakikisha maeneo waliyopewa kwa ajili ya shughuli za ufugaji wanayasimamia na kuyatunza kwa kupanda malisho na kuweka miuondombinu ya maji.

 • MKANDARASI BWAWA LA CHAMAKWEZA ATAKIWA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI NA KUZINGATIA UBORA

  MKANDARASI BWAWA LA CHAMAKWEZA ATAKIWA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI NA KUZINGATIA UBORA

  September 20, 2021

  Serikali imemtaka mkandarasi anayejenga bwawa la Kijiji cha Chamakweza kilichopo Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani, kukamilisha bwawa hilo kwa wakati pamoja na kuzingatia ubora ili liweze kuwa na tija kwa jamii ya wafugaji. Akizungumza mwishoni mwa wiki (16.04.2021 mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja kujionea ujenzi wa bwawa hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema endapo kukitokea dosari yoyote katika bwawa hilo wakati wa kipindi cha mwakwa mmoja wa uangalizi mkandarasi atapaswa kugharamia hasara zote pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.

 • KAMPUNI YA ISRAEL YAANZA MAZUNGUMZO YA AWALI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO NCHINI

  KAMPUNI YA ISRAEL YAANZA MAZUNGUMZO YA AWALI YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO NCHINI

  September 20, 2021

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amekutana na kufanya mazungumzo ya awali na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Holding ya nchini Israel Bw. Avi Postelnik yenye lengo la kuwekeza hapa nchini kupitia sekta mbalimbali zikiwemo za mifugo na uvuvi. Akizungumza jana (16.04.2021) mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yao ya awali katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam, Prof. Gabriel amesema katika mazungumzo yao wameainisha fursa kubwa zilizopo hapa nchini ikiwemo ya unenepeshaji mifugo na uongezaji thamani wa bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo.

 • PROF. GABRIEL AAGIZA UZALISHAJI WA CHANJO YA UGONJWA WA MIGUU NA MIDOMO MWAKANI!

  PROF. GABRIEL AAGIZA UZALISHAJI WA CHANJO YA UGONJWA WA MIGUU NA MIDOMO MWAKANI!

  September 20, 2021

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel ameagiza upatikanaji wa chanjo ya mifugo ya ugonjwa wa miguu na midomo (FMD) ifikapo mwakani ili bidhaa zitokanazo na mifugo ziweze kuuzwa katika masoko ya kimataifa. Prof. Gabriel ameyasema hayo jana (16.04.2021) jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), ambapo amemuelekeza Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Prof. Hezron Nonga kusimamia utekelezaji wa uanzishwaji wa chanjo hiyo ili kuwezesha viwanda vinavyozalisha nyama zitokanazo na mifugo hapa nchini kupata masoko ya bidhaa zao katika nchi mbalimbali.

 • TUTAENDELEA KUBORESHA SERA, KANUNI NA SHERIA YA UVUVI

  TUTAENDELEA KUBORESHA SERA, KANUNI NA SHERIA YA UVUVI

  September 20, 2021

  Serikali imesema ipo tayari kuendelea kupitia Sera na Sheria ya Uvuvi nchini ili iweze kukidhi mahitaji ya wavuvi wadogo kama ambavyo imekuwa ikifanya hivyo mara kwa mara pale inapohitajika. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum kutoka mkoani Kagera Mhe. Neema Lugangira ambaye alitaka kufahamu mikakati ya Serikali katika kuhakikisha Sera na Sheria ya uvuvi nchini inakidhi mahitaji ya wavuvi wadogo.

.