Albamu ya Video

 • DKT. TAMATAMAH AZUNGUMZA BAADA YA KUSHIRIKI KIKAO CHA UJIRANI MWEMA WILAYANI MWANGA.

  DKT. TAMATAMAH AZUNGUMZA BAADA YA KUSHIRIKI KIKAO CHA UJIRANI MWEMA WILAYANI MWANGA.

  September 20, 2021

  Dkt. Tamatamah azungumza baada ya kushiriki kikao cha ujirani mwema kilichojadili kuhusu ulinzi na usimamizi shirikishi wa rasilimali za Uvuvi kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu kilichofanyika wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro. (28.04.2021)

 • MIFUGO YA TANZANIA YAHITAJIKA VIETNAM NA WAZIRI NDAKI AWAALIKA WAVIETNAM KUFUGA SAMAKI

  MIFUGO YA TANZANIA YAHITAJIKA VIETNAM NA WAZIRI NDAKI AWAALIKA WAVIETNAM KUFUGA SAMAKI

  September 20, 2021

  Balozi wa Vietnam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien amesema atawasilisha serikalini vigezo vinavyopaswa kufuatwa na wafanyabishara wa hapa nchini ili waweze kusafirisha mifugo na nyama kwenda nchini Vietnam, kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji mkubwa wa nyama. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amebainisha hayo leo (28.04.2021) ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, mara baada ya kuwa na mazungumzo mafupi na balozi huyo aliyefika ofisini kwa Waziri Ndaki ili kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam na kupeana uzoefu katika sekta za mifugo na uvuvi.

 • ULEGA ATAKA KUCHANGAMKIWA KWA SOKO LA KAA NA JONGOO BAHARI!

  ULEGA ATAKA KUCHANGAMKIWA KWA SOKO LA KAA NA JONGOO BAHARI!

  September 20, 2021

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kuchangamkia fursa ya ufugaji viumbe maji wakiwemo kaa na jongoo bahari ambao wamekuwa na soko kubwa nje ya nchi. Akizungumza mwishoni mwa wiki (24.04.2021) katika Kijiji cha Tawalani kilichopo kata ya Manza iliyopo Wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo, Mhe. Ulega amesema Ukanda wa Bahari ya Hindi bado haujatumiwa vyema katika kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, hivyo wananchi kujikita zaidi katika uvuvi na kutojishughulisha na ufugaji wa viumbe maji ambao wamekuwa wakitakiwa nchi mbalimbali.

 • ULEGA - “MKIRUHUSU MIFUGO IPITE NJIA ZA PANYA NCHI ITAKOSA MAPATO”

  ULEGA - “MKIRUHUSU MIFUGO IPITE NJIA ZA PANYA NCHI ITAKOSA MAPATO”

  September 20, 2021

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka wananchi wa Kijiji cha Horohoro Kijijini Kata ya Duga katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, kutoruhusu mifugo ipitishwe kinyemela mpakani kwenda nchi jirani badala yake wawafichue wanaofanya hivyo ili kuwadhibiti kwani serikali inakosa mapato. Mhe. Ulega aliyasema hayo mwishoni mwa wiki (24.04.2021) wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo kwa kutembelea eneo lenye ekari 23 ambapo kutajengwa mnada wa mifugo kijijini hapo na kusema kuwa mnada huo utakuwa chachu ya kuinua maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

 • KIPINDI (MIFUGO NA UVUVI): MABADILIKO YA TOZO KATIKA KUKUZA SEKTA YA UVUVI

  KIPINDI (MIFUGO NA UVUVI): MABADILIKO YA TOZO KATIKA KUKUZA SEKTA YA UVUVI

  September 20, 2021

  Karibu katika makala maalum inayoandaliwa na wizara ya mifugo na uvuvi ili kukufahamisha majukumu, mafanikio, mikakati na fursa mbalimbali zilizopo kupitia wizara hii na taasisi zilizo chini yake, pamoja na kukuelimisha wewe mwananchi namna unavyoweza kujikwamua kiuchumi kupitia sekta za mifugo na uvuvi. Ninayekukaribisha katika makala hii, mimi ni edward kondela kutoka wizara ya mifugo na uvuvi ambapo katika makala hii ya leo nitakufahamisha kuhusu hatua mbalimbali za upatikanaji wa tozo mpya za ada za leseni na ushuru wa kusafirisha mazao ya uvuvi nje ya nchi.

.