Albamu ya Video

 • Dkt. Tamatamah:

  Dkt. Tamatamah: "Ninawaonya mtakaoshindwa kukamilisha miradi ya SWIOFISH mwezi Desemba 2020"

  November 30, 2020

  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah amewataka makandarasi wanaojenga ofisi za BMU katika mikoa ya Pwani, Tanga na Lindi pamoja na maabara ya utafiti wa uvuvi Tanzania jijini Dar es Salaam kukamilisha miradi hiyo mwezi Desemba Mwaka 2020. Dkt. Tamatamah amebainisha hayo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Pwani, Tanga na Dar es Salaam kukagua miradi hiyo.

 • PONGEZI KWA VIONGOZI WAKUU WA NCHI!

  PONGEZI KWA VIONGOZI WAKUU WA NCHI!

  November 30, 2020

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na taasisi zake, inatoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wake Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuaminiwa na kupatiwa ridhaa ya kuiongoza nchi kwa kipindi cha awamu ya pili ya miaka mitano ijayo. Aidha, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inampongeza Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa Rais wa nane wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar. Pia, wizara inampongeza Mbunge wa Ruangwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kuteuliwa na hatimaye kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili.

 • MAFUNZO YA WAKAGUZI WA VYAKULA VYA MIFUGO YAFUNGWA MWANZA.

  MAFUNZO YA WAKAGUZI WA VYAKULA VYA MIFUGO YAFUNGWA MWANZA.

  November 30, 2020

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo imehitimisha rasmi mafunzo ya wakaguzi wa vyakula vya Mifugo yaliyofanyika kuanzia jana hapa Mkoani Mwanza

 • WAFUGAJI WAKIJENGEWA UWEZO WATAKUZA UCHUMI WA TAIFA- MONGELA.

  WAFUGAJI WAKIJENGEWA UWEZO WATAKUZA UCHUMI WA TAIFA- MONGELA.

  November 30, 2020

  Wakaguzi wa vyakula vya mifugo leo wamepewa mafunzo yanayohusu uendelezaji wa malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo hapa mkoani Mwanza.

 • MAKALA: MAFANIKIO YA OPERESHENI SANGARA

  MAKALA: MAFANIKIO YA OPERESHENI SANGARA

  November 30, 2020

  Karibu katika makala maalum inayoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kukufahamisha majukumu na mafanikio mbalimbali ya wizara hii na taasisi zilizo chini yake pamoja na kukuelimisha wewe mwananchi namna unavyoweza kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya mifugo na uvuvi. Makala hii itakufahamisha namna serikali inavyotilia mkazo katika kudhibiti uvuvi haramu kupitia 'Operesheni Sangara' ambao umekuwa ukifanywa katika bahari na maziwa kwa kutumia vitendea kazi visivyoruhusiwa kisheria, uvuvi unaoathiri mazalia ya viumbe hai majini pamoja na kuvua viumbe maji ambavyo haviruhusiwi kisheria kutokana na umri wao pamoja uchache wao.

.
Tanzania Census 2022 Tanzania Census 2022