Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhede (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania Bw. Shigeki Komatsubara, wakati wakipandikiza vifaranga vya samaki 10,000 aina ya sato kwenye Ziwa Victoria katika Mwalo wa Shadi, Kata ya Luchelele Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, ikiwa ni ishara ya zoezi endelevu la kupandikiza vifaranga kwenye ziwa hilo na maziwa mengine. (18.09.2025)
Mkurugenzi wa Uvuvi nchini Prof. Mohammed Sheikh (kulia) akiwaonesha wananchi wanaozunguka Ziwa Ikimba lililopo mkoani Kagera ukubwa na ubora wa samaki waliopatikana mara baada ya kufunguliwa kwa ziwa hilo Septemba 12,2025.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) imewawezesha wavuvi wa dagaa waliopo eneo la Kilwa Kivinje, Lindi Chanja 40 za kisasa za kuanikia dagaa zenye thamani ya shilingi Mil. 117.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Agness Meena (kulia kwake) na baadhi ya Wakurugenzi na watendaji wa Wizara hiyo Agosti 08, 2025 muda mfupi baada ya Wizara hiyo kutangazwa vinara wa maonesho ya kimataifa ya Nane Nane mwaka 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea maelezo kuhusu matumizi ya Ndege Nyuki kwenye udhibiti wa vitendo vya uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ndani ya Viwanja vya Nnane Nane vya Dkt. John Samwel Malecela Agosti 08, 2025 jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI) Prof. Erick Komba (kushoto) kuhusu kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbari za Mifugo ili kuhamasisha ufugaji wa kisasa nchini muda mfupi baada ya kufika kwenye banda hilo Agosti 08, 2025 kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.