Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akiwalisha chakula samaki kwenye moja ya mabwawa yaliyopo kwenye kituo cha ukuzaji Viumbe Maji cha Rubambagwe kilichopo Chato mkoani Geita Januari 05,2026.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akimwagilia malisho ya Mifugo mara baada ya kufika kwenye shamba darasa la Mifugo la Bw. Shakiru Kyetema lililopo Muleba mkoani Kagera Januari 02,2026.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati) akiwalisha samaki chakula kwenye eneo la Lake Side mkoani Mara huku akishuhudiwa na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Wizara yake na Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo Desemba 22,2025.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na Naibu wake Mhe. Ng’wasi Kamani wakivuna samaki kutoka kwenye moja ya vizimba vilivyopo kwenye ziwa Victoria eneo la Lake side mkoani Mara Desemba 22,2025.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati) akimueleza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (kulia kwake) fursa zitakazotokana na Bandari ya Uvuvi wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. Nchemba bandarini hapo Desemba 19,2025, Kilwa Mkoani Lindi.
Pichani ni sehemu ya pikipiki 381 zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Maafisa Ugani nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Disemba 04,2025 jijini Dar-es-Salaam.