Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua moja ya chanjo za Mifugo mara baada ya kufika kwenye banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani Oktoba 16,2025 mkoani Tanga. Kulia anayemuelezea ni Meneja wa Wakala hiyo mkoani humo Dkt. Olivia Manangwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia moja ya pakiti za dagaa waliokaushwa kwa teknolojia ya Jua muda mfupi baada ya kufika kwenye banda la Wajasiriamali wa zao hilo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yaliyokuwa yakifanyika mkoani Tanga.
Msimamizi wa Dawati la lishe na Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Beatrice Mwijage akikabidhi mayai kwa mwakilishi wa wanafunzi wa shule ya Msingi Chuda iliyopo mkoani Tanga kwa lengo la kuhamasisha ulaji wa zao hilo la Mifugo kwa wanafunzi muda mfupi baada ya kufika shuleni hapo Oktoba 13,2025.
Bei ya Kondoo kwenye Minada ya Upili na Mipakani wiki ya Tarehe 02 Oktoba hadi 10 Oktoba 2025.
Bei ya Mbuzi kwenye Minada ya Upili na Mipakani wiki ya Tarehe 02 Oktoba hadi 10 Oktoba 2025.
Bei ya Ng'ombe kwenye Minada ya Upili na Mipakani wiki ya Tarehe 02 Oktoba hadi 10 Oktoba 2025.