WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA ILRI MIRADI YA KIMKAKATI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) Dkt. Siboniso Moyo Septemba 5, 2025, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika ulifanyika Jijini Dakar nchini Senegal.
Katika kikao hicho viongozi hao wamekubaliana kushirikiana katika kuimarisha ushiriki wa vijana kwenye miradi ya kuku, ufugaji wa samaki, uzalishaji wa chakula cha mifugo na samaki, pamoja na kushirikiana na sekta binafsi katika uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za malisho.
ILRI pia imeahidi kuiunganisha Wizara na wadau wa wengine wa maendeleo ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa kampeni ya chanjo.
Vilevile, taasisi hiyo imekubali ombi la Katibu Mkuu la kuongeza ajenda ya uvuvi katika kikao cha Mawaziri wa Mifugo kinachojulikana kama Livestock Ministerial Deep Dive” ambacho hufanyika ndani ya Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika.