Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

SERIKALI, HEIFER INTERNATIONAL KUONGEZA WIGO PROGRAMU YA BBT

Imewekwa: 13 September, 2025
SERIKALI,  HEIFER INTERNATIONAL KUONGEZA WIGO PROGRAMU YA  BBT

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, amekutana na Bi. Adesudwa Ifedi, Makamu wa Rais  wa Shirika la Heifer International anayesimamia Programu za Afrika, tarehe 5 Septemba 2025 jijini Dakar, Senegal, kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili kuhusu kupanua wigo wa Programu ya Build a Better Tomorrow (BBT) ili kuwafikia vijana wengi zaidi nchini, pamoja na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa programu hiyo, kwa lengo la kuongeza ufanisi na uendelevu wake.

Kwa upande wake, Bi. Ifedi ameipongeza Wizara kwa ushirikiano mzuri, na amemuelekeza Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania, Ndg. Mark Txoso, kuendelea kushirikiana na Wizara katika kubainisha vipaumbele vilivyojadiliwa, ili viweze kufanyiwa kazi kwa mujibu wa taratibu za shirika hilo. Vilevile, ameishukuru Wizara kwa kuitambua Heifer kama mmoja wa wadau muhimu wa maendeleo nchini.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo