Livestock Statistics

Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi ya ng’ombe baada ya Ethiopia. Takwimu za mwaka 2018/19 (NBS) zinaonyesha kuwa, Tanzania ina ng’ombe ng’ombe milioni 30.5, mbuzi milioni 18.8 na kondoo milioni 5.3, kuku wa asili milioni 38.2, kuku wa kisasa milioni 36.6, nguruwe milioni 1.9 na punda wapatao 595,160. Kaya takriban milioni 4.6 zinajihusisha na ufugaji, ikiwa ni asilimia 50 ya kaya zote nchini (National Panel Survey, 2012). Takwimu hizi zimeonyesha mifugo ni zao muhimu kwenye kuondoa umasikini

  • Uzalishaji wa maziwa lita bilioni 2.4 Aidha, usindikaji wa maziwa lita milioni 56.2 (2018 Bajeti Speech) uzalishaji wa zao la nyama tani 679,992 tani 2,608.93 za nyama (mbuzi tani 1,248.14,ng’ombe tani 1,030.79, kondoo tani 50 na punda tani 280) ziliuzwa nje ya nchi (2018, Budget Speech)
  • Usindikaji wa maziwa kwa siku (154,100 Lita) kutoka viwanda 82 wakati uwezo wa kusindika kwa siku ni lita 757,550
  • Sekta binafsi inajihusisha kuendeleza biashara kwa kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji,usindikaji na masoko ili kuendeleza Sekta ya Mifugo. Jukumu muhimu la Serikali ni kuandaa mazingira ya mazuri ya kibiashara ili sekta binafsi iweze kukua.
  • Takwimu za maziwa, nyama na mayai
  • Ulaji wa nyama kwa mwaka 2017/2018 ni wastani wa kilo 15, lita 47 za maziwa na mayai 106 kwa mtu kwa mwaka ikilinganishwa na viwango vya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO, 2011) ambavyo ni kilo 50 za nyama, lita 200 za maziwa na mayai 300 kwa mtu kwa mwaka
  • Ngozi - Mwaka 2017/2018, vipande vya ngozi zilizosindikwa hatua ya wet blue vimepungua kutoka vipande vya ngozi za ng’ombe 1,215,030 vyenye thamani ya shilingi bilioni 34.7 mwaka 2016/2017 hadi vipande 292,394 vyenye thamani ya shilingi bilioni 3.255

.