Fisheries Statistics

  • Sekta ya Uvuvi inachangia asilimia 2.2 katika pato la Taifa na imekua kwa asilimia 2.7 wavuvi na wafugaji samaki wapatao 230,977 walishiriki moja kwa moja kwenye shughuli za uvuvi.
  • Zaidi ya Watanzania milioni 4 wameendelea kupata kipato cha kila siku kwa kushiriki shughuli zinazotegemea kuwepo kwa sekta ya uvuvi ikiwemo kutengeza maboti, kushona nyavu, biashara ya samaki na mazao yake na wachuuzi Pia, katika mwaka 2017, (NBS, 2018).
  • Ukuzaji Viumbe kwenye Maji umeendelea kuhimizwa na kusimamiwa ikiwa ni pamoja na ufugaji samaki, kambamiti, kilimo cha mwani na ukuzaji wa chaza wa lulu kwa ajili ya lishe, ajira, kipato kwa nchi na kuchangia pato la Taifa. Aidha, kumekuwa na ongezeko la teknolojia za kukuza samaki wengi kwenye ujazo mdogo, hususan vizimba na ufugaji wa kutumia maji kidogo yanayozunguka na kusafishwa
  • Mwaka 2017/2018 jumla ya vizimba 315 ambavyo vilizalisha tani 1,260 vimewekwa katika maziwa ya Victoria (187), Nyasa (120) na Tanganyika (8).
  • Kilimo cha zao la mwani Tani1,329.5 zenye thamani ya shilingi milioni 469.8 zimevunwa na kusafirishwa nje ya nchi mwaka 2017/2018

.