SERIKALI KUIMARISHA MAHUSIANO NA SEKTA BINAFSI -NZUNDA

Imewekwa: Tuesday 10, May 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw.Tixon Nzunda amesema kuwa Serikali itaimarisha mahusiano na Sekta binafsi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Uwekezaji unaongezeka katika Sekta za Uzalishaji kama Mifugo, Uvuvi, Kilimo na Misitu ili kuongeza tija katika pato la Taifa.

"Lazima kama nchi tuwe na udhubutu wa kuwekeza katika Sekta za Uzalishaji kama Mifugo,Kilimo,Uvuvi na Misitu.Sekta Hizi zikiwekezwa vizuri na kusimamiwa ipasavyo zinauwezo wa kuchangia katika pato la Taifa asilimia zaidi ya 28. Hivyo sisi kama Sekta tuanze kubadilika kuwapa Elimu ya Ufugaji bora wafugi wetu."Alisema Nzunda.

Hayo ameyasema jana tarehe 22 Aprili 2022 mjini Morogoro alipokuwa akifunga mradi wa *Tajirika na Kilimo*Uliofadhiliwa na shirika la Care International Tanzania, ambapo zaidi ya wahitimu 18 kutoka Wakala ya Vyuo vya mafunzo ya Mifugo

(LITA) waliochukuliwa katika Kampasi ya Morogoro, Mpwapwa, Tengeru na Buhuri -Tanga walishiriki kikamilifu katika Mradi huo.

Aidha, nzunda amesema kuwa Ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika Sekta za uzalishaji za Mifugo,Kilimo,Uvuvi na Misitu ni muhimu kwani tayari Care International imewajengea uwezo wahitimu hao na imetoa mafunzo ya Ufugaji bora kwa vikundi 2,220 katika mikoa ya Mbeya,njombe na Iringa.

Pia, Nzunda amelitaka shirika hilo la Care International kuhakikisha kwamba linatengeneza Mkakati mahususi wa ufuatiliaji wa uendelezaji wa Mradi huo ili uendelee kuwanufaisha wafugaji na wakulima katika mikoa hiyo ambayo mradi huo ulikuwa unatekelezwa.

"Care International andaeni mkakati mahususi wa ufuatiliaji wa huu mradi na uwe mwanzo wa kuanzisha Miradi mingine katika Halmashauri na sekretarieti za Mikoa ili miradi hii iendelee kunufaisha wafugaji wetu na wakulima". Alisema Nzunda.

Vilevile Nzuda amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaendelea kushirikia na taasisi zingine za Serikali, Sekta binafsi na Wadau wengine kuboresha Kosaafu za Mifugo na kuendelea kutoa Vitendea kazi kama Magari na Pikipiki ili kurahisisha usafiri kwa maafisa Ugani walioko Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa ili kuimarisha huduma kwa Wafugaji na Wakulima.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Care International Bi.Prudence Masako amesema kuwa baadhi ya majukumu makubwa ya Care International Tanzania ni pamoja na kuwezesha Wanawake kiuchumi na kuwa na Maamuzi.

Aidha,Masako alimwambia Katibu Mkuu Mifugo kuwa asilimia 70 ya miradi Mingi inayofadhiliwa na Care International Tanzania inasaidia wanawake na Vijana kwa kutengeneza Vikundi mbalimbali na kuviwezesha katika nyanja za Ufugaji na Kilimo na tayari Care International inafanya kazi na nchi zaidi ya 90 na Makao Makuu yake yakiwa nchini Marekani.

.
Tanzania Census 2022 Tanzania Census 2022